Msimamizi Felix Brych |
Mabingwa watetezi Bayern Münich wanapimana nguvu na ManUnited huku
mafahali wawili wa Hispania Atletico Madrid na FC Barcelona wakitifua
vumbi nyumbani katika michuano ya kuingia nusu fainali za Champions
League
Watoto wa Pep Guardiola-Bayern Munich wana nafasi nzuri ya kuondoka na
ushindi nyumbani baada ya kutoka sare wiki iliyopita katika uwanja wa
Old Trafford moja kwa moja dhidi ya Manchester United.Hata hivyo ujia
unaozitenganisha timu hizi mbili ni mwembamba mno na hofu ni kubwa
tukizingatia ule ukweli kwamba tangu watawazwe mabingwa wa ligi kuu ya
Ujerumani kabla ya wakati,mabingwa hao watetezi wa kombe la vilabu
bingwa barani Ulaya -Champions League, hawajashinda tena katika medani
ya ligi kuu-Bundesliga.
Hata hivyo kocha wa Bayern Munich Pepe Guardiola anajiamini anasema:"Nna
hakika mie tutaingia nusu fainali.Tunabidi turande
ipasavyo,tutashinda.Nna hakika mie,ili kuingia nusu fainali tunahitaji
kushinda."
Hata kocha wa Manchester United Moyes anategemea kuondoka na ushindi
mjini Munich anasema:"Nnataraji tutafanya vyema zaidi kuliko duru ya
kwanza na nnamini tunaweza na ndivyo tutakavyofanya hasa .
Nani wataondoka na ushindi
Katika wakati ambapo Bayern Munich itateremka bila ya Javi
Martinez ,Bastian Schweinsteiger na Thiago,Manchester United inategemea
kumteremsha uwanjani Patrice Evra na Wayne Rooney.Wakishindwa, itakuwa
mara ya kwanza kwa timu hiyo bingwa ya Uingereza kutowakilishwa katika
kundi la nne bora katika kipindi cha miaka 23 iliyopita.
Pambano la pili leo usiku linawateremsha uwanjani mafahali wawili wa
jadi wa Hispania Atletico Madrid na Barcelona."Litakuwa pambano kali na
la kusisimua" ameungama kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone.Nani
atanyakua tiketi ya kuingia nusu fainali ya kombe la Champions League
baada ya kutoka sare moja kwa moja katika raundi ya kwanza,nasema
tusiandikie mate na wino upo.
No comments:
Post a Comment