KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, April 9, 2014

Hull City: Baraza la chama cha soka nchini England limekataa pendekezo la jina jipya la klabu ya Hull city kuwa Tigers

Jina jipya lililopendekezwa la klabu ya Hull City na kuwa Hull Tigers limekataliwa na baraza la soka la chama cha soka nchini England.
Maamuzi ya baraza hilo yamefuatia upigwaji wa kura uliofanywa na wanachama wa baraza hilo ambapo asilimia 63.5% wamepinga, hii ni baada ya pendekezo la kamati ya wanachama ya bodi ya uongozi kutaka ifanyike hivyo.

Historia ya klabu hii ilizaliwa rasmi mwaka 1904 wakati huo, wakivalia jezi za rangi nyeusi.

Mmiliki wa klabu hiyo Assem Allam, mwenye umri wa miaka 74, ambaye alitishia kuiuza klabu hiyo kama hataruhusiwa kubadilisha jina la klabu hiyo lililodumu kwa miaka 110 amenukuliwa akisema kuwa atakata rufaa juu ya maamuzi hayo.

"Endapo itakwenda vinginevyo, kama ambavyo ilivyo pitishwa na FA, huku mashabiki wakibisha, nitaachana na klabu hiyo" Allam, ambaye aliichukua klabu hiyo mwezi Disemba 2010 amenukuliwa akiongea na BBC Sport. 

Allam anaamini jina la 'Tigers' litaifanya klabu hiyo kuwa kibiashara zaidi na anadhani neno City ni la kawaida na la hasara akitumia maneno 'Lousy and Common'

Hull City fans display a banner
Mshabiki wa Hull wakionyesha kitambaa katika mchezo wa ushindi dhidi ya Liverpool mwezi Disemba ikiwa ni ishara ya kukubali klabu hiyo isalie na jina la Hull City AFC

Allam mfanya biashara mzaliwa wa Misri mwezi Agosti alitangaza jina klabu hiyo kuwa limebadilika na kuwa Hull City Tigers.
Na mwezi Disemba klabu hiyo ikapeleka pendekezo ndani ya FA kubadili jina na kuwa Hull Tigers kuanzia msimu ujao.

Allam, ambaye alijiunga na Hull 1968, alisifika sana kwa kuiokoa klabu hiyo kutokana na shida za uongozi, ambapo mwanae wa kiume  Ehab, ambaye ni makamu wa mwenyekiti wa klabu hiyo akinukuliwa mwezi huu akisema familia yake imeweka pesa nyingi ndani ya klabu hiyo kiasi cha pauni milioni £74
Msimu uliopita, Allam aliiweka katika ramani klabu hiyo kwa mara ya pili katika historia. Kwasasa wakiwa katika nafasi ya 12 katika msimamo wa Premier League na wanaweza kutinga kwa mara ya kwanza katika fainali ya FA kama watafanikiwa timu ya daraja la chini la 'League One' Sheffield United katika mchezo ambao utachezwa Jumapili ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1930.
Jina la utani la klabu hiyo "Tigers" inadhaniwa kuwa lilipendekezwa na mwandishi wa gazeti la 'Hull Daily Mail' mwaka 1905 kutokana na klabu hiyo kuvalia jezi za rangi nyeusi nakshiwa na miraba ya njano.

No comments:

Post a Comment