Mshambuliaji wa LiverpoolLuis Suarez amepewa makavu na kocha meneja wake Brendan Rodgers, kuwa afanya mazoezi peke yake kutoka na mshambuliaji huyo kuonyesha nidhamu mbaya ndani ya klabu yake.
Rodgers pia ametupilia mbali dai la mshambuliaji huyo kuwa aliahidiwa kuihama klabu hiyo majira haya ya kiangazi endapo Liverpool haitafuzu kucheza michuano ya vilabu bingwa.
Suarez mwenye umri wa miaka 26, anajipanga kuwasilisha barua rasmi ya kutaka kuihama klabu hiyo wiki hii endapo mpango wa kuelekea katika klabu ya Arsenal utazuiwa na klabu yake.
Amenukuliwa Rogers akisema
"Hakukuwa na ahadi iliyowekwa na hakuna ahadi iliyovunjwa,"
Taarifa za ndani kutoka Anfield zimesema kuwa maamuzi ya kumtaka Suarez kufanya mazoezi peke yake yalifanywa kabla ya mahojiano yake aliyofanyiwa na magazeti siku ya jumanne na yamehusishwa na mchezaji huyo kutokuwa katika shauku na michezo ya kirafiki ya hivi karibuni ambapo alikuwa akicheza katika kiwango cha chini.
No comments:
Post a Comment