KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 8, 2013

RICKIE LAMBERT AJUMUISHWA KATIKA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND.

Mshambuliaji wa Southampton Rickie Lambert ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Scotland.

Wayne Rooney naye amejumuishwa kikosini kwa ajili ya mchezo huo utakao pigwa jumatano ya Agosti 14 licha ya kukosekana katika michezo ya maandalizi ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya England akiwa na kikosi chake cha United taarifa zikiarifu kuwa mshambuliaji huyo amekumbwa na majeraha.

Rickie Lambert
Rooney ambaye ameripotiwa kutaka kuihama Manchester United kufuatia ombi la klabu ya Chelsea kutaka huduma yake inaarifiwa kuwa anasumbuliwa na bega.

Winga wa Manchester United Wilfried Zaha ameingizwa katika kikosi cha timu ya taifa akitokea katika kikosi cha pili cha wachezaji wenye umri chini ya miaka 21.

Kiungo wa Celtic Scott Brown atakuwa akikiongoza kikosi cha Scotland kitakacho kuwa kikipata nguvu nyingine kutoka kwa mshambuliaji aliyereje kutoka katika maumivu hivi karibuni Kenny Miller.

Mhsmabuliaji wa Sunderland Steven Fletcher ameachwa katika kikosi hicho kufuatia kuwa na majeraha ya kifundo.

Kuitwa kwa Lambert kunakuja katika siku ambayo mpenzi wake wa kike amepata mtoto wa kike aliyepewa jina la Bella Rose.

England squad:
 
Goalkeepers: Ben Foster, Joe Hart, John Ruddy
 
Defenders: Leighton Baines, Gary Cahill, Ashley Cole, Phil Jagielka, Glen Johnson, Phil Jones, Chris Smalling, Kyle Walker
 
Midfielders: Michael Carrick, Tom Cleverley, Steven Gerrard, Frank Lampard, Jack Wilshere, James Milner, Alex Oxlade-Chamberlain, Theo Walcott, Ashley Young, Wilfried Zaha,
 
Strikers: Jermain Defoe, Rickie Lambert, Wayne Rooney, Danny Welbeck

No comments:

Post a Comment