KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, February 28, 2014

Juan Mata & Fernando Torres nje kikosi cha Hispania kuelekea mchezo dhidi ya Italia

Mshambuliaji wa Manchester United Juan Mata na mwenzake wa Chelsea Fernando Torres wameachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kuelekea katika mchezo wa kirafiki wa Jumatano ijayo dhidi ya Italia mjini Madrid.
Mata mwenye umri wa miaka 25, alijiunga na United hivi karibuni kwa uhamisho uliogharimu pauni milioni 37 mwezi Januari, huku Torres mwenye umri wa miaka 29, yeye akiachwa kikosini licha ya kufunga goli muhimu katika machezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Galatasaray ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 Jumatano iliyopita.
"Hiki ni kikosi kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Italia na kikosi kwa ajili ya kombe la dunia" Amekaririwa Vicentre del Bosque akisema hivyo. 

Mshambuliaji wa Atletico Madrid Diego Costa amejumuishwa kikosini kwa mara ya mwanza katika kikosi cha Hispania.

Mzaliwa huyo wa Brazil ambaye ameifungia timu yake ya Atletico mabao 27.

Kikosi kamili
Spain squad to face Italy
Goalkeepers: Iker Casillas (Real Madrid), Victor Valdes (Barcelona), Pepe Reina (Napoli).
Defenders: Sergio Ramos (Real Madrid), Jordi Alba (Barcelona), Javi Martinez (Bayern Munich), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Juanfran Torres (Atletico Madrid), Raul Albiol (Napoli).
Midfielders: Xavi Hernandez, Sergio Busquets, Andres Iniesta, Cesc Fabregas (all Barcelona), Xabi Alonso (Real Madrid), David Silva (Manchester City), Thiago Alcantara (Bayern Munich), Koke (Atletico Madrid), Santi Cazorla (Arsenal).
Forwards: Pedro Rodriguez (Barcelona), Jesus Navas, Alvaro Negredo (both Manchester City), Diego Costa (Atletico Madrid).

No comments:

Post a Comment