Kikosi kamili cha mabingwa wa kombe
la Kagame Yanga ya Dar es Salaam kinaondoka nchini hii leo kuelekea nchini
Rwanda ambako kitakuwa kikiendelea na program yake ya mazoezi kwa ajili ya
maandalizi ya ligi kuu ya kandanda Tanzania bara.
Ikiwa nchini Rwanda, Yanga chini ya kocha Thom Seintfiet itacheza
michezo kadhaa ya kirafiki nchini humo kabla ya kurejea nchini kuendelea na maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom ambayo bado haijathibitishwa itaanza rasmi lini.
Jana katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Yanga ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Afrikan Lyon na kupata ushindi wa mabao 4-0 huku mabao ya Yanga yakiwekwa kwenye kamba na kiungo Harona Niyonzima aliyefunga mabao mawili
No comments:
Post a Comment