Kampeni ya
mashetani wekundu Manchester United katika ligi kuu ya kandanda nchini
Uingereza ‘Premier League’ imeanza vibaya kule Goodison Park kufuatia Everton kukomba
points zote tatu muhimu baada ya ushindi wa bao 1-0 huku shukrani zikielekezwa
kwa Marouane Fallaini aliyefunga bao zuri la kichwa katika kipindi cha pili cha
mchezo.
Kabla ya
mchezo United ilikuwa ilitangaza kuwa itamtumia mshambuliaji wake mpya Robin
van Persie ambaye alianzia katika benchi lakini Shinji Kagawa akianza katika
kikosi cha kwanza na ikiwqa ni mara yake ya kwanza kucheza ‘Priemier League’.
Tatizo kubwa
lilikuwa katika sehemu ya ulinzi ya United ambayo ilikuwa ikiwatumia Antonio
Valencia kulia na Michael Carrick alikuwa akisaidiana na Nemanja Vidic sehemu
ya ulinzi wa kati.
Everton pia
ilimpa dimba kiungo wake mpya msimu huu Steven Pienaar na Steven Naismith akisubiri katika benchi.
Kipindi cha
kwanza pale Goodison Park kilishuhudia nafasi nyingi zikitengenezwa na kila
timu huku wenyeji wakionekana kulisakama lango la United muda mwingi na kumpa
wakati mgumu mlinda mlango David de Gea ambaye alionekana kuwa bize muda mwingi.
Kunako dakika
ya 59 mpira wa kona uliopigwa toka upande wa kulia ulimkuta Fellaini, ambaye
aliruka juu na Carrick na kufanikiwa kupiga kichwa mpira uliompita De Gea na
kuandika bao pekee kwa Everton.
United
ilimuingiza Van Persie kujaribu kusaka bao la kusawazisha, lakini walikuwa ni
Everton waliokuwa wakiendelea kufanya mashambulizi ambapo Fellaini kwa mara
nyingine aliendelea kunyanyasa sehemu ya ulinzi ya United kwa kupiga kichwa
mpira mwingine ambao ulikwenda moja kwa moja kwenye mikono ya De Gea.
Dakika 10 kabla
ya mchezo kumalizika Van Persie alimpenyezea Krosi nzuri Kagawa ambayo
iliwainua mashabiki wa United vitini lakini hakufanikiwa kuandika bao.
Baada ya mchezo nahodha wa United Nimanja Vidic amesema United hawakuwa vizuri na hasa kipindi cha kwanza lakini pia kutokana na presha kubwa ya Everton hususani baada ya kupata bao ndipo hali ilipozidi kuwa mbaya zaidi.
Hata hivyo amesema United itakuwa vizuri zaidi katika mchezo ujao dhidi ya Fulham Old Trafford ambapo amesema United itakuwa ina muda wa kutosha wa maandalizi ya mchezo huo.
BOFYA HAPA
Kwa upande wake meneja wa Everton David Moyes amesema timu yake ilistahili ushindi kutokana na nguvu na uwezo walioonyesha katika mchezo huo na kwamba huo ulikuwa ni mwanzo mzuri katika hasa ikizingatiwa wameifunga timu nzuri na ngumu katika ligi.
Moyes amesema baada ya michezo angalau 10 atakuwa kwenye nafasi nzuri kuzungumzia tathmini ya kikosi chake lakini kwasasa anajipanga kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Aston Lilla kule villa park august 25.
BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment