Mshambuliaji
wa zamani wa Arsenal Eduardo ameeleza kuwa kuuzwa kwa Robin Van Persie na Alex
Song na Arsenal ni makosa makubwa “big mistake”.
Washika
mitutu hao katika siku za hivi karibuni walimruhusu mpiga mabao bora wa msimu
uliopita Robie Van Persie kujiunga na Manchester United kwa ada ya pauni
milioni £24 kabla ya kumuuza Song kwa ada ya pauni milioni £15 kujiunga na Barcelona.
Lakini mcroatia
Eduardo ambaye aliitumikia Asernal kwa miaka mitatu kabla ya kupatwa na
majeraha ya enka ambayo yalimtoa katiika kiwango na kuamua kuelekea Shakhtar Donetsk anaamini bado klabu hiyo
itarejea katika nafasi za juu.
Amekaririwa
Eduardo akisema
"ni
makosa makubwa kuwaauza wachezaji hao walikuwa muhimu sana msumu uliopita,
lakini wana wa kuwepo katika klabu kubwa za juu katika ligi”.
Kiungo nyota
mpya wa Chelsea raia wa Brazil “wonderkid Oscar” amesema kuwa atakuwa tayari
katika kikosi cha kwanza cha klabu yake hiyo mpya inayoshiriki ligi kuu ya soka
nchini Uingereza ndani ya mwezi mmoja.
Kiungo huyo
mwenye umri wa miaka 20 amejiunga na Chelsea akitokea Internacional ya Brazil
kwa ada ya pauni milioni £20 msimu huu wa uhamisho kabla ya kuonyesha kiwango
katika michuano ya Olympic 2012 jijini London akiwa na kikosi cha Brazil.
Amenukuliwa
na Radio Estadao ESPN Osker akisema
"ninajiamini
nitakuwa sawa katika kikosi hivi punde na itanisaidi kucheza na kusaka nafasi
ya kucheza katika timu".
Mbrazil huyo
alianza kuitumikia timu yake hiyo katika mchezo wa ushindi wa mabao 2-0 dhidi
ya Wigan jumapili akiingia kama mchezaji wa akiba.
Southampton wamechemka kupata saini
ya Ramirez
Southampton
imekuwa katika ushawishi mkubwa kumtaka kiungo wa Bologna Gaston Ramirez ambaye
kimsingi inaonekana jitihada zao kutokuzaa matunda hii ikiwa ni taarifa kupitia
kwa wakala wa mchezaji huyo.
Klabu yake hiyo
ya pwani ya kusini inaaminika kuwa ili kubaliana juu ya ada ya mchezaji huyo na
klabu yake pamoja na mchezaji mwenyewe siku kadhaa zilizopita lakini ombi la Southampton likatupiliwa mbali.
wakala wa
Ramirez, Oscar Betancourt amenukuliwa na mtandao wa Calciomercatoweb akisema
"mazungumzo
na Southampton yamefikia kikomo"
"Bologna
imekataa kukamilisha mpango huo bila ya “bank guarantees”. nimeongea leo na mwenyekiti
wa klabu hiyo ya Uingereza inaonekana wana angalia mchezaji mbadala.
No comments:
Post a Comment