Alex Song amekamilisha
taratibu zote za uhamisho wake kutoka Arsenal kuelekea Barcelona baada ya
kufuvu vipimo vya afya ndani ya klabu hiyo ya nchini Hispania.
kiungo huyo
wa kimataifa wa Cameroon amesaini mkataba wa miaka mitano na washika mitutu
wamepokea pauni milioni £15 ikiwa ni ada
ya uhamisho wake.
Song ambaye hakuwemo
katika kikosi Asernal kilichokwenda sare ya bila kufungana na Sunderland katika mchezo wa ligi kuu ya Engaland
uliopigwa Emirates Stadium sasa atakuwa anajiunga wa Cesc Fabregas mchezaji
mwenzake wa zamani katika klabu ya hicho kigogo cha nchini Hispania Barcelona.
Dakrari wa Barca
Ricard Pruna kupitia mtandao wa klabu amekaririwa akisema
"mwili
wa kiungo huyo hauna umeonekana kutokuwa na asilimia kubwa ya nene na pia misuli
yake iko katika kiwango kizuri.si dhani maka alishawahi kupatwa na matatizo ya
misuli tangu akiwa na umri wa miaka 17. Hizi ni taarifa nzuri . Vipimo vyote
vimekwenda vizuri na yupo kwa kocha Tito Vilanova."
Song ametengeneza mipira mingi ya mwisho
iliyozaa mabao katika Premier League kuliko mchezaji mwingine yoyote katika
klabu ya Arsenal msimu uliopita.
Kwa mantiki
hiyo Arsenal imepoteza mchezaji mchezi mbunifu katika kipindi hiki akiwa pia ni
mfungaji mzuri nyuma ya Robin van Persie ambaye ameelekea Manchester United.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amenukuliwa
akisema
"kama
unavyo fahamu klabu imekubaliana mambo kadhaa kwa ajili ya kumuuza Alex Song kwenda Barcelona.
tumefanya
hivi kwasababu tuna Jack Wilshere amerejea tunaye pia Abou Diaby back na Tomas
Rosicky tutajaribu kuleta kiungo mwingine pia."
Barca ambayo
ilimaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita katika ligi ya Hispania La Liga ilianza
vizuri msimu mpya wa ligi kwa kuwafunga mabao 5-1 Real Sociedad katika uwanja
wa nyumbani.
No comments:
Post a Comment