Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini amepigwa
marufuku mechi mbili na UEFA asisogelee eneo la kiufundi la uwanja kwa
kumlaumu mwaamuzi baada ya klabu yake kushindwa na Barcelona katika
michuano ya klabu bingwa ya Ulaya.
Pellegrini alisema baada ya timu yake kushindwa
2-0 nyumbani kwamba mwaamuzi kutoka Sweden Jonas Eriksson "hakua
mwaadilifu kwa timu zote mbili".
Alituhumiwa kwa ukosefu wa nidhamu na amepewa
adhabu ya kukaa jukwaani pamoja na mashabiki katika mkondo wa pili wa
mchuano na Barcelona mnamo Machi 12 March, poja na Mechi nyingine za
ziada.
Adhabu ya mechi moja nyingine imesimamishwa kwa miaka miwili.
No comments:
Post a Comment