Uwanja wa klabu ya AC Milan wa San Siro umefungwa kwa
mashabiki kwa mechi ijayo kama adhabu kwa matusi walioangua wakati wa
mechi hapo jana.
Hii ni mara ya pili kwa
Milan kukumbwa na hatua kama hii iliyoidhinishwa na Jaji wa Ligi ya Serie A.
Hukumu hio itaanza kwenye mechi
ijayo dhidi ya Udinese iliyopangwa tareh 19 Octoba. Pamoja na marufuku
hio klabu imetozwa faini ya takriban dola za Marekani $68,000).
Kwingine Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya
Michezl Platini amesema kua mchezo huo unafaa kuongoza juhudi za
kupambana na ubaguzi wa rangi katika michezo.
Kiongozi huyo aliyasema hayo kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa.
Mjumbe wa FIFA kutoka Afrika kusini Tokyo
Sexwale amesema kwenye mkutano huo unaojadili ubaguzi wa rangi na mchezo
wa mpira kwamba utandawazi wa vipimo vya ubaguzi wa rangi ni muhimu
katika juhudi zake kupambana na ubaguzi wa rangi.
Mwanaharakati huyo wa ANC amesema kua FIFA ina
mipango ya kuandaa mkutano wa kilele juu ya ubaguzi wa rangi kwa
ushirikiano na Wkfu wa Mandela mapema mwaka ujao.''
FIFA litatoa maelezo zaidi kuhusu mpango wake wa kupambana na ubaguzi rangi kwenye mkutano wake huko Qatar mwezi Disemba.
No comments:
Post a Comment