Klabu ya Sunderland ya Egland imemteua Kocha wa
zamani wa Brighton, Gus Poyet kuwa kocha mpya wa klabu hiyo kwa mkataba wa
miaka miwili.
Klabu hiyo ambayo inajulikana kama "The Black
Cats " inashikilia mkia katika ligi kuu ya Premier na ilimuondosha kazini Paolo Di Canio mnamo mwezi wa September baada ya kushikilia nafasi hiyo kwa mechi 13
tu.
"nina hamu ya kuwathibitishia uwezo
wangu mashabiki--ninataka wawe na imani kwa sababu tunahitaji
kushikamana " Poyet, mwenye umri wa miaka 45, ameiambia wavuti wa klabu
hiyo.
Ataungana na wasaidizi wake za zamani wa Brighton, Mauricio Taricco na Charlie Oatway.
"Nadhani msingi wa mafanikio yangu katika mechi
za nyumbani Brighton ni uhusiano wangu na mashabiki, --na naweza kuona
hali hiyo hiyo hapa ,"aliongeza Poyet, ambaye alipigwa kalamu na
Brighton mnamo mwezi wa Juni.
"ni changamoto kubwa lakini inanipa motisha na nashukuru kwa kupata fursa hii ya kuongoza katika ligi kuu"
Poyet ambaye ni mchezaji wa zamani wa taifa wa
timu ya Uruguay atakua meneja wa sita wa Sunderland katika kipindi cha
miaka mitano.
Kocha msaidizi wa Sunderland Kevin Ball amekua
akishikilia uongozi wa klabu hiyo tangu Di Canio afutwe kazi kutokana na
malalamiko ya wachezaji.
No comments:
Post a Comment