Malkia wa nyuki akiwa na Bibi Hindu ambaye
ni mwanachama wa Simba tawi la mpira pesa ndani ya ofisi za mpira pesa Magomeni usiku wa jana.Picha kwa hisani ya Rahel Pallangyor wa Lenzi ya Michezo blog. |
Mwenyekiti wa kamati ya ushindi ya Simba Rahma Al Harouz maarufu kama 'malkia wa nyuki' usiku wa jana alitembelea moja kati ya matawi yenye nguvu ya klabu hiyo tawi la mpira pesa lililoko
Magomeni Mikumi kwa lengo la kutafuta suhulu ya mgogoro uliopo kati yao
na uongozi wa Simba.
Katika safari yake kuelekea katika tawi hilo, malkia wa nyuki aliambatana na wajumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo na kufanya mazungumzo na wanachama wa tawi hilo, mazungumzo ambayo yalichukua masaa matatu.
Wanachama wa tawi la mpira pesa walitumia fursa hiyo kumpa masharti malkia wa nyuki ambapo moja ya sharti alilopewa ni kuhakikisha taratibu zilizo tumiwa na uongozi wa Simba wa kulifuta tawi la Mpira pesa wakati wa mgogoro uliopita ndizo zitumike katika kulirejesha tawi hilo.

Pili wametaka uitishwe mkutano Marchi 17 kwa ajili ya kutafuta
mstakabali wa klabu ya Simba katika kufanikisha kumalizia michezo nane
ya ligi kuu iliyobakia.
Tatu tawi hilo linamtaka Mwenyekiti Ismail Rage na yeye ajiuzulu kama walivyofanya akina Kaburu.
Kikao hicho kilifanyika kwa utulivu na kukubaliana kamati ya utendaji ya Simba inakwenda kukaa na kuyafanyia kazi ili wajenge Simba upya.

No comments:
Post a Comment