KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, November 3, 2010

Sergio Batista kuchukua mikoba ya Diego Maradona kuinoa Argentina Sergio Batista ambaye amekuwa katika benchi la ufundi la timu ya taifa ya Argentina tangu kuondoka kwa Diego Maradona ambaye mkataba wake ulimalizika baada ya kombe la dunia sasa amepewa kazi hiyo kwa minajili ya kazi ya kudumu
Batista mwenye umri wa miaka 47 aliiongoza timu ya taifa ya Argentina ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 23 katika michezo ya Olympic mwaka 2008 sasa atakuwa na mkataba mpaka baada ya kumalizika fainali za kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014.
Anakaririwa mwenyewe Batista ambaye alikuwa ni mmoja wa wachezaji katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina mwaka 1986 kikosi ambacho kilitwaa taji la dunia akisema
"ndoto yangu imetimia ilikuwa ni moja kati ya malengo yangu "
"nataka sasa kufikia malengo ya ushindi mpaka kumalizika mchezo wa mwisho wa fainali zijazo za kombe la dunia 2014 ."

Akikiongoza kikosi cha Argentina kama kocha wa muda baada ya Maradona, Batista alipata ushindi dhidi ya Jamhuri ya Ireland na Hispania pamoja na mchezo mmoja waliopoteza dhidi ya Japan.
Maradona ambaye alikuwa nahodha wa Argentina katika fainali ya mafanikio ambapo walitwaa taji la dunia mwaka 1986 nchini Mexico, alishindwa kuonyesha uwezo kama kocha miezi 20 iliyopita ambapo katika mchezo wa kombe la dunia wa robo fainali wa kombe la dunia alikubali kichapo cha aibu toka kwa Ujerumani

No comments:

Post a Comment