KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, November 3, 2010

Roy Hodgson amuomba radhi Rafael Benitez Bosi wa Liverpool Roy Hodgson ameuomba radhi kocha mtangulizi wake katika klabu hiyo ambaye kwasasa anaifundisha Inter Milan Rafael Benitez juu ya maoni yake mhispania huyo wakati akiwepo hapo kabla Anfield.
Hodgson amelazimika kufanya hivyo baada ya kukosoa uwezo wa Bernitez kushindwa kufanya matumizi sahihi wakati wake kiasi kupelekea yeye Hodgson kurithi kikosi kibovu ndani ya klabu hiyo jambo ambalo lilimlazimisha Benitez na kumuambia awajibike na kazi yake na si kuto visingizio.
Akikaririwa Hodgson amesema
"kama kauli yangu ilimkera kiasi hicho kwa kauli yangu ambayo haikuwa na maana mbaya basi kwa moyo mkunjufu nina muomba radhi."
"hakukuwa na dhamira hiyo ".
Bosi huyo wa zamani wa Fulham Hodgson alichukua nafasi ya Benitez baada ya kuanza kwa majira ya kiangazi wakati mtangulizi wake mhispania akiondoka baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 6 na kuelekea mabingwa wa Italia na Ulaya Inter Milan ambapo huko alikuwa akichukua nafasi ya Jose Mourinho ambaye kwasasa anakinoa kikosi cha Real Madria ya Hispania


Katika hatua nyingine Liverpool imemuajiri mkurugenzi wa soka wa zamani wa zamani wa Tottenham Damien Comolli kufanya kazi za kama mkurugenzi wa mikakati ya soka .
Mfaransa huyo ana umri wa miaka 38 alifukuzwa kazi na Spurs mwezi October 2008 baada ya kuitumikia Spurs kwa miaka mitatu na baadye kujiunga St Etienne ya Ufaransa kama mkurugenzi wa michezo.
Anatarajiwa kuanza kazi na mmiliki mpya wa Liverpool John Henry na meneja Roy Hodgson haraka iwezekanavyo.
Mwenyewe akikaririwa anasema
"najisikia vizuri kujiunga na Liverpool na ninacho kiangalia kwasasa ni kuangalia mbele nikishirikiana na John na Roy,"
Comolli aliwahi kufanya kazi kwa miaka saba na Asernal kama scout ndani ya Arsenal.

No comments:

Post a Comment