Lionel Messi na Cristiano Ronaldo usiku huu
walikuwa wakibadilisha kuonyesha ushujaa wao wa kupachika mabao katika mchezo
uliochezwa katika dimba la Nou Camp huku kila mmoja akifunga mabao 2 mchezo
uliozikutanisha Barcelona na Real Madrid ukiwa ni mchezo mkubwa katika soka la Hispania
maarufu kama Clasico.
Kikosi cha Tito Vilanova cha Barca kilikuwa
kikiingia katika mchezo huo kikiwa kinaongoza ligi hiyo kwa utofauti wa 8 dhidi
ya wapinzani wao wakubwa katika soka la nchi hiyo na hivyo kuendelea na rikodi
yao nzuri ya asilimia 100 baada ya michezo 6.
Alikuwa ni Cristiano Ronaldo aliyeanza
kufungua mlango wa magoli akiweka rekodi iliyotukuka ya kufunga katika kila
mchezo unaozikutanisha timu hizo na mara hii ikiwa ni mchezo wa sita mfululizo
wa Clasico ambapo amekuwa akizifumania nyavu.
Hata hivyo Lionel Messi alifanikiwa
kusawazisha kwa mpira uliorudi kwa bahati mbaya katika harakati za kuokoa na
baadaye akafanikiwa kuandika bao la pili kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja
kwa moja wavuni na kuwapa uongozi Barcelona wa mabao 2 kunako dakika ya 60 ya
mchezo kabla ya Ronaldo kusawazisha katikati ya kipindi cha pili na kuufanya
mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Kiungo wa Barca Andres Iniesta alipewa nafasi
ya kuanza katika mchezo huo hii ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu alivyofanya
hivyo kwa mara ya mwisho katika mchezo wa Supercopa dhidi ya Real mwezi August,
ilhali Adriano akisaidiana na Javier Mascherano katika sehemu ya kati ya ulinzi
kuziba mapengo ya Gerard Pique mwenye maumivu ya mguu na Carles Puyol anayesumbuliwa
na maumivu ya mkono.
Kocha wa Madrid Jose Mourinho alikifanyia
mabadiliko kikosi chake tofauti na kile kilicho ibuka na ushindi wa mabao 4-1
nyumabani kwa Ajax katika mchezo wa michuano ya ligi ya mabingwa mchezo
uliofanyika jumatano, ambapo Sami Khedira, Mesut Ozil na Angel Di Maria walichukua
nafasi za Michael Essien, Kaka na Jose Callejon.
Kwa matokeo
hayo Barcelona inaendelea kusalia katika
usukuani wa ligi hiyo wakiwa na zaidi ya points 8 kama ilivyokuwa kabla ya
mchezo ikiwa ni baada ya michezo 7.
No comments:
Post a Comment