Esperance ya Tunisia imefanikiwa kupata sare
ya bila mabao dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo katika mchezo wa kwanza wa nusu
fainali ya michuano ya vilabu bingwa barani Afrika mchezo uliofanyika usiku huu.
Mchezo huo ulikuwa ni wa kiwango sawa kiasi
matokeo ya sare kuonekana kama yalistahili.
Mazembe, licha ya kumliza mchezo wakiwa na
upungufu wa mchezaji mmoja baada ya Stopila Sunzu kutolewa kwa kadi nyekundu
iliyotokana na kupewa kadi mbili za njano.
Matokeo hayo ya leo ya Lubumbashi sasa
yataufanya mchezo wa marudiano kuwa mgumu kule Tunisia siku 14 zijazo.
Mshindi wa mchezo huo atakutana na ama Sunshine
Stars ya Nigeria au Al Ahly ya Misri katika mchezo wa fainali.
Sunshine na Ahly zilikwenda sare ya mabao 3-3
katika mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Nigeria jumamosi na hivyo kutoa
nafasi kubwa kwa mashetani wekundu wa Cairo kupenya na kutinga fainali.
TP Mazembe na Esperance zimekuwa zikigawana
ubingwa wa vilabu Afrika katika kipindi cha miaka 3 iliyopita huku Mzembe
wakichukua mara mbili 2009 na 2010.
No comments:
Post a Comment