KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, October 7, 2012

RAHA ZA MSIMBAZI ZAENDELEA BAADA YA MNYAMA KUENDELEA KUNG'ATA JKT OLJORO

Mfungaji wa mabao mawili ya Simba, kiungo Amri Kiemba akikabiliwa na mlinzi wa JKT Ruvu (Picha na Rahel Pallangyor)
Picha ya chini, mzambia Felix Sunzu akikabiliana na walinzi wa timu ya JKT Oljoro katika moja ya mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara mchezo Simba wamefanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-1 yaliyofungwa na kiungo Amri Kiemba baada ya kupokea pasi ya Edward Christopher, bao la pili likifunga pia na Kiemba baada ya mpira wake wa kichwa kushindwa kuokolewa na mlinda mlango wa OljoroShaibu Issa. Bao la tatu la Simba liliwekwa nyavuni na Emmanuel Okwi na bao nne likifungwa kwa njia ya penati na Felix Sunzu. Bao la Oljoro lilifungwa na Paulo Nonga dk 29 baada ya beki wa Simba Juma Nyoso kuanguka na mfungaji wa bao hilo kufanikiwa kumpiga chenga Juma Kaseja aliyekuja kuucheza.
Katika mchezo huo Oljoro iliwapoteza wachezaji wake wawili waliopewa kadi nyekundu Meshack Nyambele na mlinda mlango Shaibu Issa kutokana na kucheza mchezo mbaya. Mlinda mlango Shaibu ni baada ya kuudaka mguu wa Emmanuel Okwi aliyekuwa akielekea langoni kwake. 

No comments:

Post a Comment