KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, March 3, 2013

JE AZAM ITATINGA MZUNGUKO WA PILI WA MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO MBELE YA AL NASRI HUKO JUBA? MUNGU IBARIKI AZAM, MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Azam FC inashuka kwenye uwanja wa taifa wa South Sudan kukwaana na askari wa Al Nassir katika mchezo wa marudiano wa CAF Confederations Cup
Mchezo huo ambao utarushwa moja kwa moja na kituo cha Star TV kwa huko nyumbani ambao watashirikiana na South Sudan TV na kuonekana karibu Afrika nzima kupitia ving'amuzi vya DSTV-kwa Star TV na ARAB - SAT kwa upande wa South Sudan TV umevuta hisia za wananchi wengi wa hapa Juba
Azam FC leo inatarajiwa kupangwa kama ifuatavyo
Mwadili Ally, Himid Mao, Wazir Salum, David Mwantika, Jockins Atudo, Kipre Bolou, Humphrey Mieno, Salum Abubakar, John Bocco, Kipre Tchetche na Khamis Mcha Viali.
Kumbuka katika mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Azam iliibuka na ushindi wa mabao 3-1, hivyo inaweka matumaini mazuri kwa watanzania hao kuvuka hatua hii na kutinga mzunguko wa pili.

Al Nasri wanalazimika kupata ushindi wa mabao yasiyopungua mawili na huku wakilazimika kuzuia nyavu zao zisitikiswe na washambuliaji wenye uchu wa Azam kama Kipre Tcheche na John Bocco ambao wana saidiwa na Mcha Hamisi 'Vialli' na Salum Abubakar 'Sureboy'   

Mungu ibariki Azam FC, Mungu ibariki Tanzania.

No comments:

Post a Comment