Tottenham imefanikiwa kutengeneza mwanya mkubwa utofauti wa alama saba baina yake na Arsenal baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao hao wa kutoka London ya Kaskazini mchezo uliopigwa katika dimba la White Hart Lane( North London derby).
Mabao mawili yaliyofungwa ndani ya dakika mbili kabla ya mapumziko yalitosha kuwapa ushindi vijana wa meneja Andre Villas-Boas ambao sasa wamejiweka vizuri katika nafasi tatu za juu katika msimamo wa ligi kuu ya nchini Uingereza.
Wachezaji wa Spurs wakishangilia ushindi wa mabao 2-1 wa north London derby dhidi Arsenal.
Gareth Bale anavunja mtego wa kuotea uliojengwa na walinzi wa Arsenal na kuandika bao la kwanza.
Bale akishangilia goli la kwanza.
Aaron Lennon anatumia makosa ya walinzi wa Arsenal kuandika bao la pili.
Scott Parker akishangilia goli goli la pili akiwa na Aaron Lennon.
Per Mertesacker akishangilia goli pekee la Arsenal alilofunga dhidi ya Spurs.
Emmanuel Adebayor alipatwa na dhoruba na kutolewa kwa machela kipindi cha pili.
Meneja wa England Roy Hodgson na mchekeshaji Michael McIntyre walikuwa ni miongoni mwa watazamaji wa mchezo huo White Hart Lane
Mmiliki Mwanahisa wa Arsenal Alisher Usmanov naye alikuwepo White Hart Lane.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger akisalimiana na bosi wa Tottenham Andre Villas-Boas.
Bale aliwapigia makofi mashabiki wa Tottenham baada ya filimbi ya mwisho.
Jack Wilshere.
No comments:
Post a Comment