KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 1, 2013

Henrique Hilario apata mkataba mwingine wa mwaka mmoja licha ya kuachwa huru mwishoni mwa msimu uliopita

Hilario nets one-year deal as Blues perform surprise U-turn 
Hilario pichani juu atasalia Chelsea kwa mwaka wa sita baada ya kukubali mkataba wa mwaka mmoja.
 
Henrique Hilario amefanikiwa kupata mkataba mwingine wa mwaka mmoja baada ya Chelsea kubadilisha mawazo juu ya hatma yake ya baadaye.

Mlinda mlango huyo mreno alitajwa katika orodha ya wachezaji watakao achwa na The Blues kuelekea mwishoni mwa msimu uliopita lakini mwishoni mwa juma lililopita mlinda malango huyo alisafiri kuelekea nchini Marekani akiwa pamoja na wachezaji wengine wa kikosi hicho katika ziara ya maandalizi ya kuanza msimu akiwa ni sehemun ya wachezaji wa kikosi hicho chenye wachezaji  25.

Sasa bosi wa Chelsea Jose Mourinho ameamua kuchukua maamuzi ya kumzawadia mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 37 mwaka mwingine wa ziada ambaye alimsajili kutoka katika klabu ya Nacional mwaka 2006.

Akiongea na mtandao wa Chelsea Hilario amenukuliwa akisema 
‘Ni faraja kusajili mkataba mwingine wa mwaka mmoja ndani ya klabu hii, nimefarijika sana, najisikia vizuri kuwa sehemu ya kikosi bora na ninacho angalia ni kufanya kazi na Jose Mourinho.’

Mlinda mlango huyo ameidakia Chelsea jumla ya michezo 39, na kutengeneza clean sheets 18 , na nimiongoni mwa walinda mlngo wanne katika kikosi cha Mourinho akiwa pamoja na Petr Cech, Mark Schwarzer na Jamal Blackman.

No comments:

Post a Comment