Washika mitutu hao mpaka sasa wamemsajili mchezaji mmoja tu Yaya Sanogo tangu kumalizika kwa msimu uliopita pamoja na kuhusishwa na kutaka kuwachukua wakali kadha kutoka sehemu mbalimbali kama Bernard, Gonzalo Higuain na Luis Suarez.
Bosi Wenger anasema bado anaangalia nani wa kumsajili lakini amewaambia mashabiki wa klabu hiyo kuwa kikosi chake cha sasa kitapambana na changamoto ya michezo ya ligi bila hata ya kuongeza mchezaji mwingine.
‘Tunafanya kazi kwa lengo la kuimarisha kikosi, lakini tunajikita kwa vijana ambao wana nafasi hapa, ambao walianza katika ligi Premier League,
kama vile (Wojciech) Szczesny, Jenkinson, (Alex Oxlade-)Chamberlain, (Jack)
Wilshere, (Aaron) Ramsey, (Theo) Walcott jambo ambalo ni la kipekee hakuna aliyewahi kufanya hilo,’ .
No comments:
Post a Comment