Arsenal imesema wanaendelea kumpa msaada mchezaji wao wa zamani Kenny Sansom
baada ya kubainika hii leo kuwa mchezaji wao huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 54 hana sehemu ya kuishi.
Mlinzi huyo wa kushoto wa zamani wa washika mitutu hao ameweka wazi aibu yake hiyo kupitia gazeti kuwa amekuwa katika benchi katika siku za hivi karibuni baada ya kubobea katika vitendo vya ulevi na kucheza kamali.
Sansom amenukuliwa na gazeti la The Sun:
‘Nimekuwa sina mahala pa kulala kwa siku 10, kwasababu sijapata pesa , nilikuwa nakunywa , sijisikii vizuri na pia nacheza kamari. Naishi mtaani.
‘Nakunywa sana .’
Hii leo Arsenal imezungumzia juu ya kupata taarifa hiyo ya kutia aibu na kuthibitisha kuwa wao kwa kusaidiana na chama cha wachezaji wa kulipwa watatoa msaada kwa Sansom.
Msemaji wa klabu amesema,
‘Tunamfuatialia Kenny Sansom na hali yake na tumeshampa msaada na muongozo.’
Sansom aliaanza kucheza soka katika klabu ya Crystal Palace, ambako alishinda tuzo ya FA ya michuano ya vijana na ligi daraja la pili mwaka 1979, kabla ya kuitumikia Highbury kwa miaka minane.
Ameichezea Arsenal jumla ya michezo 314 na kuisaidia kushinda taji la Littlewood Cup mwaka 1987 na kuwa mlinzi wa kushoto chaguao la kwanza wa England, akiichezea jumla ya michezo 86 na alikuwepo katika fainali ya kombe la dunia mwaka 1982 na mwaka 1986 ikiwa ni pamoja na michuano ya Euro ’88.
Mzaliwa huyo wa Londoner pia amewahi kuchezea vilabu vya Newcastle, QPR, Coventry, Everton, Brentford na Watford.
No comments:
Post a Comment