MSHAMBULIAJI wa Liverpool anayegonga vichwa vya habari
kila kukicha, Luis Suarez, imearifiwa kuwa hataendelea kusalia kunako klabu hiyo
na badala yake ataamua kuhamia Arsenal, hii ikiwa kauli ya mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright.
Liverpool inashikilia msimamo wake
wa kutotaka kumuuza Suarez kiasi cha kuwafurusha mara mbili Arsenal na ofa ya
kutaka kumsajili mchezaji huo, anayetaka kujiunga na klabu inayoshiriki ligi ya
mabingwa ulaya msimu huu.
Suarez raia wa Uruguay nchi ambayo
imepitisha muswaada wa kuhimiza wananchi kulima kwa wingi zao la
bangi, ameshaweka wazi kuwa anataka kuondoka Liverpool licha kuingia kandarasi
ya muda mrefu na klabu hiyo tangu mwaka, 2012.
Ian Wright, anaamini kuwa ofa mpya ya
pauni milioni 41 iliyotolewa na Arsenal itaweza kumfanya suarez kukubali
kujiunga na wabeba mitutu hao wa London, lakini Liverpool inataka kumruhusu
mchezaji huyo kuondoka endapo itajitokeza klabu yenye uwezo wa kulipa pauni
milioni 50.
………………………………
Katika hatua nyingine Liverpool, imetoa
ofa ya pauni milioni £21kuelekea katika klabu ya Atletico
Madrid ya Hispania, kwa lengo la kumsajili mshambuliaji wao Diego Costa.
Ofa hiyo inaaminika kuwa huenda ikakubaliwa
na uongozi wa Atletico Madrid na kumruhusu Costa, 24 kuondoka,na kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers,anamatumaini kuwa
watakamilisha dili hilo bila matatizo.
Costa, ambaye ni raia wa nchini
Brazil, alijiunga na Atletico Madrid mwaka 2010 akitokea klabu ya Valladolid, na
amefanikiwa kufunga mabao 10 kwenye michuano ya ligi kuu ya Hispania msimu uliopita.
...........MWISHO.......
MOHAMED KALLON AENGELUWA UCHAGUZI WA URAIS WA SOKA NCHINI SIERA LEONE.
Shirikisho la mpira wa miguu duniani Fifa, limekubaliana
na uamuzi wa kuenguliwa kwa Mohamed
Kallon na watu wengine wawili, Rodney Michael na Foday Turay, katika kinyang’anyiro
cha urais wa shirikisho la kandanda la Sierra Leone.
Hii inamaanisha kuwa, mwana mama Isha
Johansen, aliyetimiza vigezo vyote vinavyohitajika katika kuwania nafasi
hiyo, atakuwa mgombea pekee wa urais wa shirikisho hilo la mpira nchini Siera
Leone, na atakuwa Rais wa kwanza mwanamke kuongoza shirikisho hilo.
Uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo nchini sierra
leone, SLFA,unataraji kufanyika mapema kesho jumamosi.
Mohamed Kallon,ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Inter Milan na AS
Monaco, ameenguliwa katika kinyang’anyiro hicho baada ya shirikisho kujiridhisha
kuwa hakuwepo nchini humo kwa zaidi ya miaka 5, ikiwa ni sifa moja wapo
inayohitajika kuwa mgombea wa nafasi hiyo.
Hata hivyo Kallon, mwenyewe amekanusha madai
hayo akisema kuwa hayana ukweli wowote na maamuzi hayo ni uonevu mtupu kwake.
...................MWISHO..............
The Cranes kujipima kwa Mapharao wa Misri.
Timu ya taifa ya Misri
itakutana uso kwa uso dhidi ya timu ya taifa ya Uganda 'The cranes', katika mchezo
wa kimataifa wa kirafiki utakaopigwa tarehe 14 ya mwezi huu, mchezo ambao kwa
timu zote mbili utatumika kama maandalizi ya michuano ya kufuzu kombe la dunia.
Mchezo huo utafanyika katika mji wa Pwani wa El Gouna, kilometa 430 toka jijini Cairo, kutokana na kuepuka vurugu za vuguvugu la kisiasa na kiusalama.
Makamu wa rais wa shirikishao la soka nchini Uganda, Mujib
Kasule, amesema mchezo huo ni muhimu ili kujiweka fiti kwa timu zote mbili na
kutoa nafasi kwa makocha kuona mapungufu ya vikosi vyao.
Naye kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uganda,
Milutin 'Micho, amethibitisha kuwa mchezo huo utaisadia kuiwashia taa ya kijani
kuelekea katika michuano ya kombe la dunia.
The Cranes ipo katika nafasi ya pili kwenye
kundi lao ikiwa na pointi 8, ambapo italazimika kuwafunga vinara wa kundi, Senegal
tarehe 7 mwezi September, mchezo ambao utafanyika mjini Marrakech, nchini Morocco.
Wakati wamisri wao, tayari wakiwa wamefuzu katika raundi inayofuata ya michuano ya kufuzu
kombe la dunia mwakani, baada ya kujinyakulia pointi 15 kwenye kundi lao la G, wakati
nafasi ya pili ikishikiliwa na Guinea yenye pointi 10.
............MWISHO.........
SOLDADO ANASEMA SI RAHISI KUCHEZA NA GARETH BALE
Mchezaji mpya aliyesajiliwa na klabu
ya Tottenham
Hotspur, Roberto Soldado, amekiri kuwa hatarajii kucheza pamoja na
kiungo Gareth Bale, kwa kuwa mchezaji huyo safari yake imeiva.
Tottenham Hotspur imemsajili Soldao
kwa ada ya kuvunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo ,pauni milioni £26m,ili
kuimarisha safu yake ya uishambuliaji kabla ya kuanza michuano ya ligi.
Soldado,amesema anapenda kuona
anakwenda kwenye timu Spurs ambayo Bale anacheza,lakini asingependa kuona
wanapangwa pamoja.
Soldado aliyetokea klabu ya Valencia,alijiunga
na klabu hiyo akitokea Getafe miaka mitatu iliyopita amefanikiwa kufunga mabao 80 katika mechi 146,ikiwemo magoli 24 aliyoyafunga
msimu uliopita wa ligi ya La Liga.
Anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa
na Spurs katika usajili huu wa majira ya joto,na atakamilisha zoezi hilo la
usajili wake leo ijumaa baada ya kufanyiwa vipimo vya afya yake.
Wachezaji wengine waliosajiliwa na
Spurs majira haya ya joto ni pamoja na kiungo Paulinho toka klabu ya
Corinthians ya brazil kwa ada ya pauni milioni £17m,pamoja na Nacer Chadli toka
klabu ya FC Twenty kwa ada ya karibu pauni milioni £7m.
Kocha mkuu wa klabu ya
Valenci,Miroslav Duckic,amesema uongozi wa klabu yake baada ya kushindwa
kuipata saini ya mshambuliaji wa Aresenal,Olivier Giroud na mshambuliaji wa
klabu ya Real Zaragoza-Helder Postiga,umeamua kuelekeza juhudi zao kuifukuzia
saini ya Fernando torres wa Chelsea.
.........Mwisho..........
REDKNAPP ANASEMA HATA KAMA UNAMTAKA REMY KWA MKOPO LIPA KWANZA PAUNI MILIONI 2
Kocha wa klabu ya QPR, Harry Redknapp, amesema klabu yeyote itakayojitokeza kutaka
kumchukua mshambuliaji wao Loic Remy kwa
mkopo, italazimika kuweka mezani pauni milioni £2m.
Tayari Newcastle united,ipo katika mazungumzo na QPR,kuhusu
mchezaji huyo aliyejiunga nao tangu mwezi januari kwa ada ya pauni milioni £8m.
‘huyu ni mchezaji ambaye tumekubaliana kuwa
tutamtoa kwa mkopo,lakini klabu ambayo inahitaji huduma yake ni lazima itoe
pauni milioni mbili,lakini kama ipo klabu inayotaka kumnunua moja kwa moja basi
italazimika kutoa pauni milioni £8million.
.......MWISHO........
RONALDO KUMBE NI KIRAKA NDANI YA MADRID.
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema
kuwa mshambuliaji wake nyota Cristiano
Ronaldo, anaweza kucheza katika nafasi yeyote atakayoitaka,hii ni katika kile
kinachoonekana klabu hiyo kutaka kumbakiza asiondoke.
Taarifa za mwisho jioni hii zinasema, tayari
mabingwa wa England Manchester united, wameanza mazungumzo na uongozi wa Madrid ili
kumrejesha Ronaldo Old Trafford.
Lakini kocha Ancelotti, aliyechukua mikoba ya
kukiongoza kikosi hicho hivi karibuni, anahaha kutaka kumbakisha ronaldo lakini
kama ataamua kuondoka, basi atalazimika kuingia katika vita ya kumfukuzia kiungo
wa Tottenham, Gareth Bale ili amjumuishe kwenye kikosi chake .
..........MWISHO.......
BALE BADO KIDUCHU KUTUA MADRID
Klabu ya Tottenham inakaribia kabisa
kukubali kumuuza nyota wao anayekipiga pia na timu ya taifa ya Wales, Gareth Bale,kwa dau la pauni milioni
105 ambalo Real Madrid,wamekubali kutoa.
Kocha wa klabu ya Real Madrid, Carlo
Ancelotti, amethibitisha kuwa klabu yake ipo katika mazungumzo mazito na ya
mwisho kabisa na uongozi wa Tottenham,kuhusu dili hilo.
Bale, 24,yupo chini ya uangalizi wa
madaktari ambao wanampatia matibabu madogo baada ya kuumia,na huenda akakosa
mechi mbili za mwisho za kujiandaa na msimu wa ligi kuu.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment