Na. Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Usajili
wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) sasa utafungwa
Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3 mwaka huu kama
ilivyokuwa imepangwa awali.
Uamuzi
wa kusogeza mbele umetokana kuchelewa kupata disc ya usajili msimu huu
ambayo ndiyo inayotumika kwa usajili wa elektroniki unaofanywa kwa
wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom. Disc hiyo ambayo hutolewa na
kampuni ya NAS Technology ya Tunisia tayari imeshawasili.
Kutokana
na mabadiliko hayo, sasa kipindi cha pingamizi kitakuwa kati ya Agosti 6
na 12 mwaka huu wakati Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itakutana
Agosti 13 na 14 mwaka huu kupitia na kufanyia uamuzi usajili wa
wachezaji wenye matatizo.
Hatua
ya pili ya usajili itaanza tena Agosti 15 mwaka huu ikihusisha
wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu
huu. Timu zitakazoruhusiwa kusajili ni zile ambazo zitakuwa hazijajaza
nafasi zote za usajili. Dirisha dogo za usajili litafunguliwa kuanzia
Novemba 15 mwaka huu hadi Desemba 15 mwaka huu.
Pia
klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zinapowasilisha usajili wao zinatakiwa
kuambatanisha nyaraka zinazoonesha viwanja vyao vya mazoezi, nakala za
bima kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi. Masuala hayo yameelezwa
kwenye Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom
KAMISHNA RWIZA KUSIMAMIA MECHI YA CHAN
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Alfred Rwiza wa Tanzania kuwa
kamishna wa mechi ya raundi ya pili ya michuano ya kuwania tiketi ya
kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).
Rwiza
atakuwa kamishna katika mechi ya kwanza ya raundi hiyo itakayohusisha
mshindi wa mechi kati ya Msumbiji na Namibia dhidi ya Angola
itakayochezwa kati ya Agosti 9 na 11 mwaka huu. Mechi hiyo itachezeshwa
na refa Noram Matemera kutoka Zimbabwe.
Matemera
atasaidiwa na Wazimbabwe wenzake Tapfumaney Mutengwa atakayekuwa
mwamuzi msaidizi namba moja, Ncube Salani ambaye ni mwamuzi msaidizi
namba mbili wakati mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Ruzive Ruzive.
No comments:
Post a Comment