Ligi kuu ya
soka nchini Kenya “Kenyan Premier League (KPL)” imeanza tena hapo jana hatua ya
mzunguko wa pili kwa Nairobi City Stars kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Thika
United ushindi ambao umekuwa ni wanne mfululizo kwa upande wao.
Bao la
washindi liliwekwa kimiani na George Mwangi kunako dakika ya 12 baada ya mlinda
mlango wa Thika
Joel Batari kushindwa
kuushika mpira wa nguvu uliopigwa na David Kingatua.
Baada ya ushindi huo City Stars imepanda mpaka
nafasi ya 10 ikikusanya jumla ya points 20.
Kwingineko Mathare
imeichapa Karuturi Sports ya Naivasha kwa jumla ya mabao 3-1 katika mchezo wao wa kwanza wa mzunguko wa
pili.
Mathare
ilionyesha nia ya kushinda tangu mapema kwa kufanya mashambulizi ya mara kwa
mara. Juhudi zao zilizaa matunda kunako dakika ya 14 kupitia kwa Francis Ouma ambaye
alikuwa mwiba baada ya kross ya Jesse Were.
Dakika ya 29
Ouma akatoa pasi murua kwa Were ambaye alifumga bao la pili.
Kipindi cha pili dakika ya tano Were alikuwa katika nafasi nzuri na hakufanya
ajizi baada ya kupokea pasi ya toka kwa Andrew Tololwa ,
Bao la Karuturi la kufutia machozi liliwekwa
kimiani kunako dakika ya 90 na Jacob Omondi akifunga kwa kichwa pasi ya Geofrrey
Msiebe.
Upande wao Gor Mahia wamewachapa Western Stima
kwa bao 2-1 katika mchezo mwingine uliopigwa Mumias Sports Complex,
Mabao ya
washindi yalifungwa na Joseph Njuguna and Dan SSerunkuma.
No comments:
Post a Comment