Wote wanafuraha: Barcelona wamekuwa katika maandalizi mazuri ya kuanza msimu huku Suarez akiwa katika mazoezi ya binafsi |
Luis Suarez
ametanabaisha ya kuwa amefurahia sana kurejea katika mazoezi baada ya hii leo Ijumaa kujiunga na wachezaji wenzake kwa mara ya kwanza na klabu yake mpya ya Barcelona.
Raia huyo wa Uruguay alikuwa akifanya mazoezi ya peke yake wakati akisubiri kusikilizwa kwa rufaa yake ya kumng'ata kwa meno mlinzi wa timu ya taifa ya Italia Giorgini Chiellini katika michuano ya kombe la dunia.
Wakati akiendelea kusimama kwa adhabu ya miezi minne na michezo tisa ya kimataifa, mahakama ya kimataifa ya michezo ya (Court for Arbitration in Sport) iliyo na makao yake nchini Uswiz imesimamisha kuendelea na shauri lake huku ikipunguza kifungo cha kutokujishughulisha na jambo lolote linalo husu mchezo wa soka na kumuweka huru kushiriki mazoezi na klabu yake ya Barcelona na kushiriki michezo ya kirafiki mpaka Oktoba.
Suarez anatarajiwa kuimarisha safu ya ushambuliaji ya Barcelona mara baada ya adhabu yake kumalizika mwezi Oktoba
Suarez alionekana akiwa mwenye tabasamu kubwa akiungana na wachezaji wenzake wa Barcelona siku ya kwanza ya mazoezi
Hapa kazi tu: Luis Suarez akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Barcelona ijumaa ya leo pamoja na nahodha Xavi
Amenukuliwa akisema
' Nina furaha sana na kuhisi kama ni mchezaji wa soka kwa mara nyingine na kuungana na wachezaji wenzangu katika mazoezi'
CAS wamemruhusu Luis Suarez kuunga na kikosi cha katika mazoezi na michezo ya kirafiki lakini hakupunguziwa adhabu.
No comments:
Post a Comment