Aliyekuwa kocha wa Yanga Saintfiet |
Karibuni
katika mkutano mfupi ambao unalenga kuzungumzia ama kuelezea masikitiko makubwa dhidi ya Kocha wa Timu ya
Yanga TOM SAINTFIET aliyoyatoa kwa vyombo vya habari kuidhalilisha hoteli yangu juu ya huduma zake na kiwango chake alichokiita cha
huduma
mbovu!.
Kimsingi
management ya Peter safari’s Hotel
na Uongozi wa chama cha wamiliki wa Mahotel Mkoa wa Mbeya, tumesoma na
kusikiliza kwa masikitiko makubwa lawama zilizotolewa na Kocha huyo kuwa “hajawahi
kulala kwenye hoteli ya hadhi ya chini kama hii katika nchi 20 alizowahi kufanya kazi katika nchi za Afrika”.
Uongozi
wa hotel na chama cha wamiliki wa
hotel kwa ujumla kinachukulia suala hili kama kampeni maalumu ya kudhalilisha
na kukatisha tamaa wateja kuiona mbeya haina hotel za hadhi za kuishi timu na
watu wenye hadhi katika jamii, kitu ambacho si kweli na ni visingizio kutokana
kushindwa kwake kuwezesha timu kufikia matarajio ya mashabiki na wapenzi wa timu hiyo.
Kimsingi
viongozi wa Timu ya yanga waliomba kuwalaza wachezaji wawili katika kitanda
kimoja tofauti na taratibu za hotel na hii ilitokana na mipangilio yao hasa
kwenye suala la uwezo wa kulipia kila mchezaji chumba chake, aidha, uongozi wa
hotel ulijitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuhakikisha kuwa wachezaji wanapata
huduma walizohitaji na hata wakati mwingine kutoa usafiri kwaajili ya kununua
mahitaji ya familia zao kitu ambacho hakifanyiki maeneo mengine kwa gharama za
hotel.
Kwa
kutambua madhara yaliyotokana na matamshi ya kocha huyo raia wa Ubelgiji,
Uongozi wa hotel ya Peter Safaris
unayaona matamshi haya kama udhalilishaji mkubwa na wenye nia mbaya ya kuuharibia mkoa
wa mbeya na kuutangaza vibaya kwa
wageni juu ya uwezo wake katika utoaji
wa huduma za hoteli.
Aidha kwakuwa maneno ya kocha huyo yametamkwa na kutangazwa kwenye vyombo
vya habari pasipo kukanushwa na viongozi wa Timu ya Yanga ambao ndiyo
waliofanya maandalizi na kufanya mazungumzo ya maombi ya kuwalaza wachezaji wawili katika vyumba ambavyo vina
uwezo wa kulaza mtu mmoja (single), Peter safaris inaliona jambo hilo kama ni
sehemu ya kashfa iliyojengwa kwa nia ya kuiharibia hotel biashara na kuipotezea hadhi mbele ya
wageni na watumiaji wa huduma za
PETER SAFARIS ambayo inaendelea
kupanua huduma zake kwa mkoa wa mbeya na maeneo mengine.
Ikumbukwe
kuwa Peter safaris hotels imekuwa ikipokea wageni wa hadhi mbalimbali wakiwemo
viongozi wa ngazi za kitaifa, wageni kutoka nje wa hadhi za juu na
wafanyabiashara wakubwa, hivyo ugeni wa Yanga na hadhi inayozungumzwa na Kocha
huyo hauwezi kufikia mahala pa kuidhalilisha hotel kwa kiwango hicho ambacho
kocha huyo amevitumia vyombo vya habari licha ya hotel kutopata maoni yoyote
baada ya timu kuhudumiwa kwenye sanduku la
maoni(suggestion box).
Kutokana
na hali hii iliyojitokeza, uongozi wa Hotel unautaka uongozi wa Yanga kuiomba
radhi management ya Hotel ya Peter safaris kwa lugha ya kashfa na isiyoendana
na utamaduni wa Mtanzania kwakuzingatia kuwa wachezaji wakiulizwa namna
walivyohudumiwa wasingeweza kuzungumza hayo ambayo mwalimu wao ameyazungumza
kwa utashi wake.
PETER
SAFAR’s inalichukulia jambo hili kwa uzito unaostahili kwakuzingatia kuwa lugha iliyotolewa na mteja wake huyo
imevuka kiwango cha kuvumilika, na njia pekee ambayo tunadhani ni ya uungwana
kabla ya kuingia kwenye taratibu za kisheria ni kuwataka YANGA kuomba radhi kwa
lugha ya dharau na kashfa dhidi ya hotel yetu vinginevyo tunakusudia kuchua
hatua za kisheria kwa kuzingatia kuwa hotel inaendeleshwa kwa mujibu wa
taratibu na sheria zinazotawala huduma za hotel na zile za mipango miji
ambazo
masuala ya usafi ni miongoni mwa maeneo muhimu ya kukidhi viwango vya
uendeshaji wake.
Ninawashukuruni
kwa mahudhulio yenu
Nawasilisha
MKURUGENZI MTENDAJI
PETER
SAFARI’s HOTEL
MBEYA.
No comments:
Post a Comment