KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, June 20, 2012

KANU MBIYAVANGA MLOKOLE WA SIMBA AWATAKA WACHEZAJI KUWA NA MUNGU.

Kanu mbiyavanga akiwa amevaa Rosali kubwa ishara ya mapenzi yake kwa mungu.

 Kiungo mpya wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya kandanda ya Tanzania Bara  Simba ya jijini Dar es Salaam Kanu Mbiyavanga  amewaka wachezaji wenzake wa Simba kuwa karibu na mungu kila mara kwani hakuna jambo linalo kwenda bila ya Mungu

Akizungmza na Rockersports amesema yeye binfsi ni Mlokole na amekuwa akitembea na mungu kila mara na kumuomba wakati wote jambo ambalo analifanya hata anapokuwa na familia yake.

Amesema yeye na familia yake hutumia muda mwingi kuimba nyimbo za kumsifu mungu kabla ya kulala na kufanya maombi nyakati za usiku kwa kuwa anaamini kila jambo linahitaji kumtanguliza mungu kwanza.

Kanu Mbiyavanga akiwa katika jumba la mazoezi ya viungo akijiweka fiti.

Amewataka wachezaji wenzake kumjali kwanza mungu wataona mambo yakiwanyookea
Mchezaji huyo aliyesajiliwa na Simba msimu huu akitokea DC Motema Pembe ya DRC Congo ni baba wa watoto wawili mmoja akiwa na umri wa miaka minne na mwingine miaka miwili amesema ana mpenda sana mkewe ambaye amekuwa akitembea naye kila sehemu na sasa wanaishi pamoja maeneo ya Keko juu Changombe jijini Dar es Salaam.

Mke wa Kanu Mbiyavanga akiwa baby wake
 Kuhusu soka amesema amedhamiria kucheza soka ya kiwango cha juu ili kukidhi matarajio ya klabu yake ambayo imeonekana kuwa na matumaini na yeye.
Kanu ambaye kwasasa ameanza mazoezi na wachezaji wenzake katika uwanja wa sigara maeneo ya Chang'ombe Temeke jijini Dar es Salaam amesema amefurahishwa na ushirikiano ambao ameanza kuupata toka kwa wachezaji hao ambao amewasifia kuwa na uwezo mkubwa wa kucheza soka.
Kanu amesema kwasasa mbali ya mazoezi ya kawaida pia hufanya mazoezi ya viungo nyakati za asubuhi kwa lengo la kujiweka fiti zaidi.
Kanu Mbiyavanga akiwa na Blogger wa Rockersports nyumbani kwake maeneo ya Chang'ombe

No comments:

Post a Comment