Mabingwa watetezi wa michuano ya taifa ya vijana wachezaji chini ya umri wa miaka U-17 Copa Coca-Cola Kigoma wamewataka mashabiki wake na wenyeji wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi June 24 katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo ambapo watetezi hao watakuwa wakianza kutetea taji lao dhidi ya
Lindi.
Akizungumza na ROCKERSPORTS toka Kibaha mkoani Pwani katibu wa chama cha kandanda mkoa wa Kigoma Mrisho Bukuku amesema timu yake imewasili jana ikiwa salama na wachezaji wake wanahari kubwa ya kutete taji lao.
Michezo
mingine katika siku ya ufunguzi itakuwa ni Morogoro washindi wa pili wa mwaka
jana dhidi Manyara mchezo ambao utapigwa katika viwanja vya Tanganyika
Packers Kawe ilhali Kinondoni wakianza
dhidi ya Temeke katika uwanja wa Nyumbu Kibaha na Kilimanjaro wakianza na Kusini Unguja katika uwanja wa Tamco huko Kibaha.
Tayari makocha 35 wa vikosi vya timu za Copa
Coca-Cola wameshapata semina ya FIFA ya namna ya kutoa mafunzo iliyoendeshwa na
wakufunzi wa FIFA na CAF Ulric Mathiot kutoka Seychelles na Sunday Kayuni wa
Tanzania.
Wachezaji vijana wa michuano ya copa coca-cola wakifualia michuano mwaka jana |
Jumla ya mikoa 28 ya kisoka iko katika
maandalizi ya mwisho mwisho na mikoa ikitarajia kuwasili jijini Dar es Salaam
kuanza michuano hiyo ya 6 tangu kuasisiwa kwake.
Timu
zimegawanywa katika makundi manne huku kila kundi likiwa na timu saba.
Watetezi wa taji Kigoma wapo katika kundi A
pamoja na mikoa ya Arusha, Ilala, Kusini Pemba, Lindi, Rukwa na Ruvuma.
Kundi B kuna
mikoa ya Iringa, Kaskazini Pemba, Manyara, Mjini Magharibi, Morogoro, Mwanza na
Tanga.
Kundi C kuna
mikoa ya Dodoma, Kaskazini Unguja, Kinondoni, Mara, Mbeya, Mtwara na Temeke wakati
ambapo kundi D linajumuisha mikoa ya Kagera, Kilimanjaro, Kusini Unguja, Pwani,
Shinyanga, Singida na Tabora.
Timu mbili
za kwanza kutoka kila kundi zitaungana kwa pamoja katika hatua ya robo fainali.
Mchezo wa
fainali unatarajiwa kuchezwa July 15
TFF kupitia
mwenyekiti wa soka la vijana Msafiri Mgoyi amesema mchezaji halali katika
michuano hiyo anatakiwa awe amezaliwa kuanzia January 1, 1996.
Kigoma ilishinda
taji hilo baada ya kuichapa Morogoro katika mchezo wa fainali ulichezwa katika
uwanja wa karume.
No comments:
Post a Comment