Manchester City inaendelea kumfukuzia mlinda mlango wa Malaga Willy Caballero.
Taarifa zinasema kuwa City ilijipanga kunasa saini ya mlinda mlango huyo wakati wa kipindi cha uhamisho wa kiangazi kilichopita baada ya kuthibitishwa na Caballero mwenyewe mwezi uliopita.
Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 32 amekuwa sana katika fikra za meneja Manuel Pellegrini na akimchukulia kama ni mtu mwenye mwendo mzuri.
City inataka kuwepo na ushindani kwa Joe Hart ambaye amekuwa katika misimu tofauti.
Willy Caballero lifahamika kwa Manuel Pellegrini kwasababu walikuwa pamoja katika klabu ya Malaga.
Joe Hart
Muajentina Caballero amenukuliwa akisema
‘Nimeongea na Pellegrini kabla hajaondoka Malaga.
Najua nia yake ya kunichukua lakini sikujua kama angeendelea na walinda mlango aliokuwa nao au kunichukua.’
Pellegrini
No comments:
Post a Comment