Mshambuliaji wa washika bunduki wa
London Arsenal ya nchini England Olivier Giroud, amesema kuwa goli la mapema
katika mchezo wao dhidi ya Bayern Munich ni muhimu, ili kufanikisha mpango wao kupata
matokeo mazuri ya kusonga mbele kwa hatua ya robo fainali ya michuano ya vilabu
bingwa Ulaya usiku wa leo.
Washika bunduki hao wamesafiri
kuelekea Allianz Arena nchini Ujerumani wakiwa nyuma kimatokeo, ambapo
wanalazimika kubadilisha matokeo ya kuwa nyuma kwa 3-1 dhidi ya Bayern Munich, ambao tangu mwezi Oktoba hawajapoteza mchezo.
Giroud, bila kujali nafasi ya Arsenal
ilivyo kwasasa, amesema kuwa ameangalia aina ya uchezaji wa Bayern Munich na anadhani
Munich maarufu kama ‘Bavarians' wanafungika.
Giroud ambaye hajafunga katika
michezo sita ambayo Arsenal imekuwa ikicheza ugenini, anaamini anaweza kufanya
hivyo dhidi Bayern hii leo kufuatia kauli ya nyota wa Munich Thomas Mueller kusisitiza
kuwa hawatacheza mchezo wa kujilinda kwa kuwa wako mbele kimatokeo.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
Mlinda mlango wa Chelsea Thibaut Courtois anogewa na Atletoco Madrid.
Thibaut Courtois amethibitha juu ya
matamanio yake ya kuendelea kusalia na Atletico Madrid msimu ujao badala ya
kurejea katika klabu yake aliyokulia ya Chelsea ya England.
Raia huyo wa Belgiam katika kampeni ya misimu miwili
iliyopita, alikuwa na klabu hiyo yenye maskani yake katika mji mkuu wa Hispania
wa Madrid, klabu ambayo ilifanikiwa kushinda mataji mawili ya Europa League na UEFA
Super Cup ikiwa ni pamoja na kucheza fainali ya Copa del Rey.
Courtois mpaka sasa bado hajaichezea klabu
yake iliyomkuza ya Chelsea ambayo alimsaini kutoka katika klabu ya Genk
inayoshiriki ligi ndogo inayotambulika kama Jupiler Pro League mwaka 2011.
Mlinda mlango huyo mwenye umri wa
miaka 21 ametanabaisha kuwa hana haraka ya kurejea Stamford Bridge na kuwa kama
mlinda mlango namba mbili Petr Cech.
Aidha Courtois, ambaye ameweka rekodi
ya kucheza dakika 820 bila kuruhusu goli kabla ya mchezo wa Jumapili ambapo
walipoteza dhidi ya Real Sociadad kwa bao 1-0, amesema anajua kuwa hatma yake
baadaye iko nje ya maamuzi yake
Amenukuliwa akisema
"Nina furaha, nafurahia maisha
hapa na wenzangu katika kikosi. Si maamuzi yangu , Chelsea na Atletico wnapaswa
kuongea".
@@@@@@@@@@@@@@@
Bosi wa Liverpool
anasema kiangazi ni kusaka Ubora na wingi.
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amesisitiza
kuwa klabu yake itakuwa ikisaka ubora na sio ujazo wakati atakapo kuwa katika
kazi kuboresha kikosi chake wakati wa soko la wachezaji la kipindi cha
kiangazi.
Kwasasa wekundu hao wako katika
mwendo mzuri wa ushindi baada ya kushinda michezo yao mitatu ya mwisho ya ligi
kuu ya England ‘Premier League’ huku Manchester United na Tottenham wakifanya
vema kwa kukusanya alama zaidi tangu kuanza kwa mwezi Desemba.
Rodgers anaamini kuwa kuongezeka kwa Daniel
Sturridge na Phillippe Coutinho mwezi Januari kumeongeza nguvu na uhai ndani ya
kikosi na kusisitiza kuwa ongezeko la wachezaji wenye ubora katika kipindi cha
majira ya kiangazi kutarejesha changamoto mpya ya kiushindani zaidi katika
nafasi za juu.
"Tunasaka ubora sasa na si
uwingi"
"Tunaona matokeo ya ubora wa Coutinho
na Sturridge, hicho ndicho tunachokitafuta. Endapo tutawaleta wengine watatu au
wanne wa kiwango hicho, tukichanganya na hao tulionao tutakuwa na kikosi cha
nguvu ambacho kitaweza kushindana"
Rodgers alivurugwa na jaribio la kumchukua
Clint Dempsey kushindikana msimu wa kiangazi uliopita, timu ya utafutaji wa wa wachezaji kitasaidia kuleta wachezaji wa
kweli wakati huu.
Anaamini kuwa Liverpool iko sawa
katika kila idara na itaendelea kuongeza vipaji.
@@@@@@@@@@@@@@@
Mikel Arteta ataka Arsenal kuwekeza majira ya kiangazi kama wanataka mataji.
Kiungo nyota wa klabu
ya Arsenal, Mikel Arteta anaamini kuwa kunatakiwa kufanyika uwekezaji wa
kutosha katika kipindi cha majira ya kiangazi kama klabu hiyo inataka kutafuta
mataji tena msimu ujao.
Baada ya timu hiyo
kung’olewa katika Kombe la Ligi na Bradford City na lile la FA na Blackburn
Rovers timu hiyo imekosa matumaini ya kunyakuwa taji lolote msimu huu ikiwa
imepita miaka nane toka walipofanya hivyo mwaka 2005.
Arteta anafikiri kuwa
pengo kati ya vinara wa Ligi Kuu nchini Uingereza Manchester United na timu
hiyo ni kubwa na kuonya kuwa bodi lazima igundue kuwa wanaporomoka kutoka
katika ushindani kabla hawajachelewa.
Nyota huyo aliendelea
kusema kuwa klabu hiyo ina msingi mzuri kuliko klabu yoyote ambayo amewahi
kucheza na pia mfumo mzuri, wachezaji wazuri na fedha za kutosha ambazo
wanaweza kufanya chochote hivyo haoni sababu kwanini klabu hiyo inasuasua
badala ya kutumia nafasi hiyo kuwa kileleni.
Wachezaji wengi nyota
huvutiwa kwenda katika klabu ambayo watapata uhakika wa kucheza michuano ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya hivyo hivyo Arteta anaamini kama Arsenal itakuwa
ikishindwa kushika nafasi nne za juu ni wazi inaweza kuporomoka kiushindani
kama ilivyokuwa hapo awali.
@@@@@@@@@@
Franz Beckenbauer anasema Pep Guardiola anachangamoto kubwa ya mafanikio Bayern Munich.
Nguli wa soka wa
zamani nchini Ujerumani, Franz Beckenbauer amedai kuwa meneja mtarajiwa wa
klabu ya Bayern Munich Pep Guardiola atakuwa chini ya shinikizo kubwa kufikia
mafanikio yaliyowekwa msimu huu na meneja wa sasa Jupp Heynckes.
Kocha huyo wa zamani
wa Barcelona anatarajiwa kuchukua mikoba ya kuinoa Bayern Julai mosi mwaka huu
lakini Heynckes ambaye ataondoka mwishoni mwa msimu ametengeneza pengo kubwa
katika mbio za ubingwa wa Bundesliga kitu ambacho kinamuogopesha Beckernbauer.
Bayern kwasasa
inaongoza Bundesliga kwa tofauti ya alama 20 baada ya kupambana kutoka nyuma
mara mbili na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Fortuna Duesseldorf
Jumamosi iliyopita.
Klabu hiyo kama
ikishinda mechi tatu za ligi zinazofuata itakuwa tayari wametawazwa mabingwa
wapya wa Bundesliga hiyo ikiwa ni mara ya 23 kushinda taji hilo.
Nguli huyo anadai kuwa
kila mtu anafikiri mambo yanaweza kubadilika kwa klabu hiyo wakati Guardiola
atapoanza kufundisha hivyo kama timu itachukua ubingwa kwa tofauti ndogo ya
alama kuliko msimu huu watu wanaweza kukosa imani naye.
Maneno ya nguli huyo
yaliungwa mkono pia na rais wa Bayern Uli Hoeness ambaye amesema anafikiri timu
hiyo itakuwa bingwa wa ligi msimu huu hivyo shinikizo kwa Guardiola na klabu
litakuwa kubwa.
@@@@@@@@@@@
Gennaro Gattuso kustaafu rasmi kiangazi.
Kiungo nyota wa zamani
wa kimataifa wa Italia na klabu ya AC Milan, Gennaro Gattuso amesema anatarajia
kustaafu rasmi kucheza soka katika kipindi cha majira ya kiangazi ili aweze
kuhamishia nguvu zake kwenye ukocha.
Gattuso mwenye umri wa
miaka 35 ambaye kwasasa anacheza katika klabu ya FC Sion ya Switzerland amedai
anadhani wakati wa kutundika daruga umefika baada ya kucheza kwa kipindi cha
miaka 18.
Nguli huyo amesema
mara baada ya kuacha kucheza soka anataka kujitolea kwa nguvu zake zote katika
kazi yake mpya ya ukocha ili aweze kupata mafanikio kama ilivyokuwa wakati
akicheza soka.
Nyota huyo aliendelea
kudai kuwa amepata uzoefu wa kutosha wakati akiwa mchezaji chini ya makocha
Marcello Lippi na Carlo Ancelotti kwani walikuwa walimu wazuri kwake wakati
akiwa Milan.
FC Sion ambayo kwasasa
inashika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Switzerland maarufu
kama Swiss Super League wanatarajia kusafiri kwenda Geneve Jumapili kupambana
na timu ya Young Boys.
@@@@@@@@@@
No comments:
Post a Comment