Gokhan Gonul wa
Fenerbahce akiwa amelala chini kifudifudi kuzuia damu kuendelea kutoka
baada ya kukumbana na dhoruba la kupigwa na mguu wa kichwa.
|
Brave Gokhan Gonul alilazimika wa Fenerbahce amejikuta akingoka meno katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Europa League.
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 28 alipigwa kichwani alipokutana na mguu wa kushoto wa Nicolas Gaitan wakati akipiga mpira katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Estadio da Luz.
Gokhan alilazimika kupumzika kwa dakika chache akiwa uwanjani huku damu nyingi zikitoka mdomoni kabla ya kuondolewa kwa machela
Taarifa kutoka vyombo vya habari vya Uturuki zimesema kuwa mlinzi huyo aliyekimbizwa hospitali amepoteza meno yake kadhaa.
Katika mchezo huo Fenerbahce walijikuta wakipoteza mchezo wakifungwa kwa mabao 3-1 na Benfica.
Gaitan ndiye aliyefungua kitabu cha magoli kabla ya Dirk Kuyt kusawazisha lakini magoli mawili ya Oscar Cardozo yakaipeleka Benfica fainali baada ya kushinda kwa mabao 3-2 ukiwa ni ushindi wa jumla.
Sasa Wareno hao watakutana na Chelsea mjini Amsterdam May 15 kufuatia kikosi cha Rafa
Benitez kuichapa Basle 3-1 katika mchezo mwingine wa nusu fainali na kushinda ushindi wa jumla wa mabao 5-2.
Gonul akipakiwa katika machela.
No comments:
Post a Comment