Kocha Stewart Hall akisalimiana na wachaji wake. |
Kocha mkuu wa Azam fc Stewart John Hall amesema ni kosa kubwa kwa timu yake kupoteza alama hata moja katika mfululizo wa michezo yake ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara na kwamba katika mchezo wa leo ushindi ni muhimu.
Alitoa kauli hiyo mara baada ya mchezo wa kimataifa wa kombe la shirikisho dhidi ya Al Nasr ya Juba ambapo Azam ilishinda kwa mabao 3-1 kwamba wanarejea katika ligi wakiwa na malengo ya kushinda kila mchezo ikiwemo michezo miwili ya ligi kuu baina ya JKT na Yanga mwishoni mwa juma.
Kauli hiyo ya Stewart Hall inaonyesha wazi kuwa Azam fc imejipanga kuikandamiza JKT Ruvu katika uwanja wake wa nyumbani Chamazi jioni ya leo na kuikamata Yanga ambao ndio vinara wa msimamo wa ligi wakiwa na alama 36 kileleni.
JKT Ruvu ambayo haijafanya vizuri msimu huu kulinganisha na minne
iliyopita chini ya kocha wake Charles Kilinda inakamata nafasi ya nne
kutoka chini ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi 15 itakuwa na dhamira ya kuinyesha Azam uwezo na ubora wa soka yao inayosifika lakini pia kutokana na matokeo mazuri.
Iwapo
itafanikiwa kushinda mechi hiyo, Azam itaendelea kujiimarisha katika
nafasi ya pili nyuma ya vinara Yanga. Azam ambayo ni moja ya timu zenye
safu kali ya ushambuliaji katika
ligi hiyo ikiwa imefunga mabao 27 ina
pointi 33.
Mshambuliaji John
Bocco na Waziri Salum tayari wamerejea uwanjani na wapo fit kwa ajili ya mikiki ya ligi hiyo mchezo huo utapigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi saa 10 kamili
jioni!
Mchezo mwingine ni Kule jijini Mbeya ambapo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Simba baada ya kwenda sare michezo miwili mfululizo, jioni ya leo wanashuka Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya wakiwa wageni wa Tanzania Prisons.
Baadhi ya wachezaji wa Simba. |
Katika
mechi zake mbili zilizopita, Simba iliondoka pointi mbili tu kati ya
sita ilizokuwa ikizipigania. Ilitoka sare na timu za JKT Ruvu kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na baadaye sare ya 1-1 ugenini dhidi ya
Oljoro JKT.
Hiyo
itakuwa mechi ya nne kwa Mfaransa Patrick Liewig tangu aanze kuinoa
Simba huku akifanikiwa kuondoka na ushindi katika mechi moja dhidi ya
African Lyon inayokamata mkia kwenye ligi hiyo. Simba iliilaza Lyon
mabao 3-1.
Kwa
upande wa kocha Jumanne Chale anashusha kikosi chake uwanjani leo akiwa na kumbukumbu nzuri ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya
African Lyon katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja huo huo Februari 9
mwaka huu.
Hekaheka
nyingine itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wenye uwezo wa
kuchukua watazamaji 25,000 utakapokuwa mwenyeji wa mechi kati ya Toto
Africans na African Lyon. Wakati Lyon ikikamata mkia, Toto Africans
yenye pointi 14 inashika nafasi ya 12 katika ligi hiyo inayoshirikisha
timu 14.
Kikosi cha Coast Union. |
Mwamuzi
Simon Mberwa wa Pwani atakuwa shuhuda wa mechi kati ya Coastal Union ya
Tanga na Oljoro JKT ya Arusha itakayofanyika Uwanja wa Mkwakwani jijini
Tanga. Mechi hiyo inatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na
uimara wa timu zote mbili.
Kumbuka Coast bado inaugulia maumivu ya kufungwa na Kagera Sugar katika mchezo wao wa mwisho hivyo itahitaji ushindi katika uwanja wake wa nyumbani ili kurudisha imani kwa mashabiki wake wa mkoani Tanga.
No comments:
Post a Comment