Mshambuliaji
Muller akiuangalia mpira aliopiga na kumpita mlinda mlango wa Arsenal
kwa juu na kutinga wavuni huku mlinda mlango huyo Wojciech Szczesny asijue la kufanya.
|
Hatma ya Arsene Wenger ndani ya klabu ya Arsenal bado inaendelea kuwa mashakani kufuatia vijana wake kutoteshwa na Bayern Munich katika mchezo uliopigwa katika dimba la nyumbani Emirates Stadium ambapo sasa inaonekana dhahiri shahiri kuwa wako njia moja kutolewa katika kinyanganyiro cha ligi ya mabingwa Ulaya.
Washika bunduki hao sasa wa wanahitaji miujiza katika mchezo wa marudiano utakao pigwa nchini Ujerumani March 13 endapo watataka kusonga mbele na kuondoa tofauti ya mabao mawili yanayo wafanya wawe nyuma ya Bayern Munich baada ya matokeo ya leo ya kichapo cha mabao 3-1.
Mabao ya Munich yaliyo fungwa na Toni Kroos, Thomas Muller na Mario Mandzukic yalistahili kuwapa ushindi wageni kutokana na mchezo wao wa malengo waliokuwa wakionyesha usiku huu.
Mabao ya Munich yaliyo fungwa na Toni Kroos, Thomas Muller na Mario Mandzukic yalistahili kuwapa ushindi wageni kutokana na mchezo wao wa malengo waliokuwa wakionyesha usiku huu.
Lukas
Podolski aliifungia Arsenal goli na kufanya matokeo kuwa 2-1 na hivyo kuwapa uhai kimchezo baada ya kufunga goli la kichwa uliotokana na mpira wa kona mpira ambao ulimpita mlinda mlango Manuel Neuer lakini hata hivyo washambuliaji wa Beyern walikuwa bado wana njaa na goli la Mario Mandzukic lilizima matumaini ya mzee Wenger ya kupata bao la kusawazisha na hivyo kunusuru kibarua chake.
Toni Kroos akifunga goli la kwanza kwa shuti kunako dakika ya saba ya mchezo.
Kiungo wa kimataifa wa Ujerumani Tony Kroos akishangilia bao la kwanza.
Jack Wilshere akijibishana na Kroos kufuatia kumfanyia madhambi Santi Cazorla.
Thomas Muller (katikati) akimalizia mpira wa kutemwa na mlinda wa Arsenal na kufanya matokeo kuwa 2-0.
Per Mertesacker (katikati) akionyesha kulikataa goli la akidhani alikuwa ameotea.
Arsene Wenger na msaidizi wake Steve Bould wakiangalia namna kikosi chao kinavyombwela.
Arsenal iliwakilishwa na
Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Vermaelen, Arteta, Wilshere, Ramsey (Rosicky 71), Cazorla, Podolski (Giroud 71), Walcott.
Arsenal iliwakilishwa na
Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Vermaelen, Arteta, Wilshere, Ramsey (Rosicky 71), Cazorla, Podolski (Giroud 71), Walcott.
wachezaji wa akiba,
Mannone, Diaby, Oxlade-Chamberlain, Coquelin, Jenkinson.
Goals: Podolski 55.
Waliopigwa kadi,
Sagna, Vermaelen, Arteta, Ramsey, Podolski.
Bayern Munich iliwakilishwa na,
Neuer, Lahm, Van Buyten, Dante, Alaba, Javi Martinez, Schweinsteiger, Muller, Kroos (Gustavo 73), Ribery (Robben 83), Mandzukic (Gomez 78).
Wachezaji wa akiba
Starke, Shaqiri, Rafinha, Tymoschuk.
Goals: Kroos 7, Muller 21, Mandzukic 77.
Waliopigwa kadi
Lahm, Muller, Schweinsteiger.
Referee: Svein Oddvar Moen (Norway)
Attendance: 59,974
Mannone, Diaby, Oxlade-Chamberlain, Coquelin, Jenkinson.
Goals: Podolski 55.
Waliopigwa kadi,
Sagna, Vermaelen, Arteta, Ramsey, Podolski.
Bayern Munich iliwakilishwa na,
Neuer, Lahm, Van Buyten, Dante, Alaba, Javi Martinez, Schweinsteiger, Muller, Kroos (Gustavo 73), Ribery (Robben 83), Mandzukic (Gomez 78).
Wachezaji wa akiba
Starke, Shaqiri, Rafinha, Tymoschuk.
Goals: Kroos 7, Muller 21, Mandzukic 77.
Waliopigwa kadi
Lahm, Muller, Schweinsteiger.
Referee: Svein Oddvar Moen (Norway)
Attendance: 59,974
Lifeline: Lukas Podolski (kulia) akishangilia na Per Mertesacker baada ya kufunga bao pekee la Arsenal katika kipindi cha pili.
Podolski akitumia vizuri makosa ya mlinda mlango Manuel Neuer na kuukwamisha mpira wavuni.
Wamiliki nao walikuwepo jukwaani Alisher Usmanov (kushoto) na Stan Kroenke walikuwepo jukwaani.
Mashabikiwa wa Bayern wakishangilia kwa fataki na kupuliza puto kabla ya mchezo.
Bastian Schweinsteiger (wa pili kushoto) na Philipp Lahm wakizuia shuti la Santi Cazorla.
Schweinsteiger alilambwa kadi ya njano na mwamuzi Svein Oddvar ambayo itamgharimu kukosa mchezo mmoja.
No comments:
Post a Comment