Shrikisho la soka duniani FIFA limepitisha matumizi ya
kutumia teknolojia ya kuthibitisha mpira kuvuka mstari na kuingia golini ( Goal-line Teknoloji 'GLT') katika
fainali ya kombe la dunia nchini Brazil 2014.
Teknoloji hiyo pia imethibitishwa kuwa itatumika katika
michuano ya kombe la shirikisho ambayo itaanza kutimua vumbi June 15 mwaka huu.
Taarifa iliyochapishwa katika mtandao wa shirikisho hilo imesema
"Baada ya jitihada za kuhakikisha teknolojia hiyo
inajaribiwa na kuona kama inafaa kupitia michuano ya kombe la dunia la vilabu
nchini Japan Desemba mwaka jana 2012, FIFA imeamua kuanza kutumia GLT katika
michuano ya kombe la shirikisho nchini Brazil june 2013 and baadaye fainali ya
FIFA ya kombe la dunia 2014 nchini Brazil.
Imekaririwa taarifa hiyo ikisema
"Lengo ni kutumia GLT ili kusaidia waamuzi na kupanda
mfumo katika viwanja vyote”
FIFA pia imezindua zabuni ya imealika watu wote wenye
kutengeneza na kutoa huduma ya mfumo huo wa goal-line
technology kuomba kupewa kandarasi hizo huku maamuzi ya aliyeshinda
yakitarajiwa kutolewa mwezi April.
Mifumo ya Hawk-Eye na GoalRef yote tayari imepitishwa
na FIFA, ambayo inatumia kamera
ikihusisha nguvu ndogo za mafasa ya kunasa nguvu za sumaku kuzunguka goli
ambapo ndani ya mipira kutakuwa na saketi inayowashwa kwa lengo la kunasa
mawasiliano(siyo tafsiri rasmi).
Alves anamtaka Neymar ajiunge na Barcelona.
Mlinzi wa kimataifa wa Brazil na Barcelona Dani Alves amemtaka
mshambuliaji wa Santos na timu ya taifa ya Brazil kujiunga naye katika timu yake ya
Barcelona wakati huu ambapo kuna tetesi kuwa kigogo hicho cha Hispania
kinatengeneza mazingira mazuri ya kujenga hatma njema ya baadaye ya
kinda huyo.
Neymar amekuwa mchezaji bora kwa miaka miwili mfululizo wa
bara la Amerika Kusini.
Alves alishindwa kuficha juu ya hisia zake katika jaribio lake la kuendelea kumshawishi
Neymar mwenye umri wa miaka 20 kujiunga Nou Camp.
Lakini wakati tetesi nyingine juu ya mshambuliaji huyo
kutaka kuelekea Ulaya baada ya michuano ya kombe la dunia mwakani na kujiunga
na Manchester City au Bayern Munich kama
ilivyokuwa inaarifiwa , Alves anasema atahakikisha mipango hiyo inashindwa.
No comments:
Post a Comment