Hii
ni picha ya Floyd Mayweather aliyoiweka katika mtandao wa kijamii wa
Twitter jana jumanne akionyesha rekodi yake ya kushinda jumla ya mataji
nane ya uzito tofauti tano.
|
Floyd Mayweather Jnr atatatea taji lake la ubingwa wake wa WBC uzito wa welterweight dhidi ya Robert Guerrero pambano ambalo litafanyika May 4 huko Las Vegas.
Raia huyo wa Marekani ambaye apigiki, baada ya kutumikia kifungo cha jela kwa miezi miwili kufuatia kumjeruhi mpenzi wake wa zamani mwaka jana, amekuwa nje ya ulingo tangu alipokutana na Miguel
Cotto May mwaka jana.
Mayweather, mwenye umri wa miaka 35, amekubali kucheza mapambano ya maonyesho sita katika kipindi cha mkataba cha miezi 30 ikiwa ni mkataba ambao unachukua nafasi ya showtime za HBO (pay-per-view broadcaster).
Akiwa amepigana mara tano katika kipindi cha miaka 5 iliyopita, haitakuwa jambo la kushangaza kumuona bondia huyu(pound-for-pound) akitimiza masharti ya mkataba wake mpya alioingia hivi karibuni.
Na kama atatimiza hilo itakuwa ni mkataba mkubwa kuliko yote iliyowahi kusainiwa na bondia kwa mujibu wa taarifa zinavyosema.
Akikaririwa na ESPN mshauri wa Mayweather Leornard Ellerbe amesema,
'Floyd
amesaini mkataba wa kuvunja rekodi na Showtime PPV/CBS na Floyd ni mwenye kwasasa ni mwenye furaha isiyo kifani'.
'Unbeaten' Mayweather akishangilia pamoja na mashabiki wake katika moja ya mapambano.
No comments:
Post a Comment