KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, February 20, 2013

BAADA YA KUSHINDA TAJI LA BRAZIL OPEN, RAFAEL NADAL AJIFANANISHA NA RONALDO DI LIMA.

Fan: Former footballer Ronaldo (left) watched Rafael Nadal with Brazilian mixed martial artist Anderson Silva
Mchezaji wa zamani wa Brazil Ronaldo (kushoto) akimuangalia Rafael Nadal akiwa na msanii Anderson Silva.

 Rafael Nadal amesema amejifunza kutoka kwa mkongwe Ronaldo de Lima ambaye alirejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi wa kipindi kirefu na kuendelea kupata mafanikio.

Kauli ya Nadal inafuatia ushindi wa taji wa la Brazil Open aliloshinda huku Ronaldo akiwa ni mmoja wa watazamaji jumapili iliyopita ambapo kabla ya hapo alikuwa majeruhi kwa kipindi cha miezi saba akisumbuliwa na mguu wa kushoto.
 Nadal amesema sasa anataka kuendeleza rekodi ya mafanikio aliyoyapata nchini Brazil na kufanikisha hilo kwa kufuta nyayo za mkongwe huyo wa soka wa Brazil licha ya kupata majehara makubwa. 
Nadal amesema  
'Ronaldo ni mfano mkubwa kwangu wa kuiga kwa kuwa mafanikio yalikuja baada ya majeraha makubwa ambayo yalitishia fani yangu'
 Licha ya kushinda taji hilo la Brazil Open bado mhispania huyo anasumbuliwa na mguu ambao bado haujapona vizuri lakini anaamini kwa kuwa ameshinda taji mbele ya Ronaldi basi hiyo ni ishara kuwa atapona na huo mwanzo mwingine mzuri katika fani yake.
Ronaldo alimaliza safari yake ya kucheza soka akiwa mshambuliaji mkubwa duniani baada ya kuwa katika kirefu cha  takribani miaka mitatu ya maumivu ya mguu kiasi kupelekea kufanyiwa upasuaji.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona, Real Madrid, Inter Milan na AC Milan alishinda mataji mawili ya kombe la dunia akiwa na Brazil na anaendelea kushikilia rekodi ya kufunga magoli 15 ya michuano hiyo.
 Nadal alimshinda mchezaji bora namba 3 wa dunia wa mchezo huo David Nalbandian wa Argentina 6-2, 6-3 Jumapili na kutwaa taji lake la 51 katika mchezo wa tennis.
Road to recovery: Nadal found some form in Sao Paulo yesterday
 Taste of victory: Nadal bites the trophy of the Brazil Open after beating David Nalbandian Road to recovery: Nadal found some form in Sao Paulo yesterday

No comments:

Post a Comment