Shirikisho la soka duniani Fifa linatarajiwa kukubaliana juu ya kuhamisha michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 kutoka katika utamaduni wake wa kikalenda lakini ikiwa ni baaada ya majadiliano makali kuendelea kuchomoaza.
Bosi wa Fifa Sepp Blatter anataka bodi ya uongozi ya Fifa kupiga kura juu ya maamuzi ya kubadilisha kalenda katika kikao cha wiki hii cha siku mbili kilicho anza hii mjini Zurich.
Wakati upinzani ukiendelea kushamiri juu ya sakata hilo inavyoonekana maamuzi ya kuhamisha kalenda huenda yakachelewa.
Hofu ni juu ya kile ambacho kitatokezea wakati wa joto kali la kiangazi kwa wachezaji na mashabiki na ikitakiwa sasa wakuu na wadau wengine kufikia kwa mara nyingine tena juu ya hilo.
Blatter alikaririwa akisema mwezi Agosti kuwa angependelea kuhamia mwezi Januari kutoka mwezi Juni kwa lengo la kuepukana na joto kali la zaidi ya nyuzi joto 40C huko katika nchi ya Ghuba.
Lakini Rais wa Uefa Michel Platini ni miongoni mwa wajumbe wengi wa kamati ya utendaji ya Fifa ambao wanahitaji mazungumzo zaidi na wadau wa mchezo huo kabla ya kupiga kura.
Mkutano wa siku mbili wa kamati ya uatendaji umeanza hii leo ambapo maandalizi ya michuanoa ya kombe la dunia nchini Brazil na sakata hilo la Qatar na michuano ya mwaka 2022 ni Agenda kubwa zitakazo jadiliwa.
Agenda ya Qatar itajadiliwa hapo kesho Ijumaa.
Mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa, Fulham, Manchester United na Everton Louis Saha ni miongoni mwa wadau wanaopinga michuano hiyo kuchezwa Kiangazi huko Qatar.
No comments:
Post a Comment