KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, November 30, 2013

Michael Laudrup: Hatuogopi vipigo vya Manchester City wanapokuwa Etihad tutawashangaza.

 Meneja wa Swansea City Michael Laudrup anasema kwa kujiamini kuwa kikosi chake kitakuwa kikiumana dhidi ya City kikiwa katika hali nzuri na kamwe hawaiofii timu hiyo kuelekea katika mchezo wao wa ligi hapo kesho Jumapili

Kikosi cha Manuel Pellegrini kimeshinda michezo yote sita ya ligi ya Premier katika uwanja wa nyumbani ikishinda magoli ya idadi ya kuvuatia takribani 26 katika mfululizo wa michezo hiyo.

Katika michezo yao miwili iliyopita katika uwanja wa Etihad Stadium, Manchester City walishinda kwa matokeo ya magoli sita na saba dhidi ya Tottenham na Norwich kila moja.

Hata hivyo Laudrup anasisitiza kuwa kikosi chake kinaweza kikaonyesha maajabu na kushinda dhidi ya City ikiwa ni tangu wapande daraja la Premier League.

"Huwezi kucheza na hofu katika soka. lazima uweke heshima kwa kila mtu yule aliye juu na aliyechini lakini usihofu kamwe" Dane alikuwa akiongea na waandishi wa habari.

"Ni timu bora inapokuwa uwanja wa nyumbani katika ligi hivyo tunajua utakuwa ni mchana mgumu lakini tunaweza kushangaza pale.

"Kila mmoja anategemea City kushinda kwa idadi kubwa ya mabao kwakuwa walifanya hivyo hivyo kwa timu kadhaa wakiwemo Manchester United and Tottenham.

Swansea imeshinda michezo mitatu ugenini nje ya Liberty Stadium msimu huu lakini City ndio kigogo cha kwanza chenye kupewa nafasi ya taji kukutana nayo miongoni mwa vigogo wengine wanaopewa nafasi kama hiyo.

No comments:

Post a Comment