![]() |
Li Na raia wa China aliye anza vizuri Wimbledon |
Mashindano
ya tennis ya Wimbledon nchini Uingereza yameanza hii leo huku wachezaji mahiri
wanaoshiriki wakiwemo kama Novak Djokovic kutoka Jamhuri ya Serbia, Maria
Sharapova ambaye ni raia wa Urusi na Roger Federer kutoka Uswisi.
Kati ya
wachezaji ambao mambo yameanza kuwaendea vyema hii leo ni Mchina Li Na, ambaye
moja kwa moja ameingia raundi ya pili ya mashindano, kwa kumuondoa Ksenia
Pervak wa Kazakhstan 6-3, 6-1.
Baada ya
kuondolewa mapema katika mashindano ya French Open katika raundi ya nne, Li Na anaonekana
ameongeza juhudi za kufanya vyema katika mapambano ya Wimbledon.
Hata hivyo alimzidi
nguvu Pervak, mwenye umri wa miaka 21, na kumfunga mapema akitumia muda chini
ya saa moja.
Sasa Li Na
atakutana na Sorana Cirstea kutoka Romania, au Mfaransa Pauline Parmentier,
katika raundi ya pili.
Venus Williams aanza hovyo mzunguko
wa kwanza wa Wimbledon
![]() |
Venus Williams akifuta machozi baada ya kuharibu round ya kwanza Wimbledon |
Bingwa mara
tano wa michuano ya Wimbledon Venus Williams anasema hafikiriii kuacha kucheza licha
ya kupata kichapo cha kwanza mshituko toka kwa Elena Vesnina katika mzunguko wa
kwanza wa michuano hiyo.
Mmarekani huyo
mwenye umri wa miaka 32 ambaye alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Sjogren's
Syndrome(hali ya kuwa na maumivu katika nyama na mwili kukauka) alifungwa kwa 6-1
6-3 na raia wa Russian Elena ambaye ni namba 79 kwa ubora duniani.
Amenukuliwa akisema
"haiwezekani
nakwenda kufikria na kupiga moyo konde"
Williams
alimudu kuzuia mara moja tu na kutupa hovyo katika set ya kwanza.
No comments:
Post a Comment