KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, October 26, 2010

Final bet: Oracle Paul the Octopus picks Spain over Netherlands to win W...

The Octopas Paul” pweza paul ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kwa utabiri wake wa michezo kadhaa ya timu ya taifa ya Ujerumani na hata mchezo wa fainali wa kombe la dunia amefariki dunia.
Inaarifiwa pweza huyo alizaliwa mwezi January 2008 huko Weymouth nchini Uingereza kabla ya kuhamia nchini Ujerumani alikuwa ni mtabiri mkubwa katika fainali za kwanza kufanyika barani Afrika zilizo fanyika nchini Afrika kusini.
Alitabiri sawa bin sawia matokeo ya michezo miwili ya Ujerumani katika michuano ya Euro 2008 na kushindwa kufanya hivyo katika michezo ya mingine ya vipigo vya nchi hiyo toka kwa Croatia na Hispania.
Katika summer's World Cup mwaka huu alifanikiwa kwa asilimia 100% kutabiri baada ya kufanikiwa kufanya vema matokeo yote ya Ujerumani kabla ya kufanikiwa tena matokeo ya mchezo wa fainali yake ambapo Hispania walifanikiwa kuichapa Uholanzi kwa bao 1-0 na kutawazwa taji la kombe la dunia.
Pweza Paul alikuwa akifanya hivyo kwa kuchagua aina ya chakula kilichokuwa kimewekwa katika moja ya boksi ambapo linakuwa limeviringwa na bendera ya nchi husika.
Stefan Porwoll meneja wa “Oberhausen Sea Life Centre” kituo kinacho hifadhi viumbe vya baharini nchini Ujerumani ambacho kilikuwa kikimuhifadhi Pweza Paul
Anasema
"tunaweza kusema kuwa kwa uwezo wetu na ufahamu wa kutosha alikuwa akifurahia maisha mazuri hapa kufuatia uangalizi mkubwa aliokuwa akipewa na timu ya watu maalum hapa
"mafanikio yake ni zaidi ya hata kombe la dunia lenyewe ,tumeamua kumpa eneo dogo maalumu atakapo zikwa na kulifanyia uangalizi wa kudumu pakiwa ni pa kisasa na kupendeza wakati wote.
Mmiliki wa pweza huyo aliwahi kugomea offer mbalimbali za watunzi wa vitabu baada ya kombe la dunia na kumtaka aingizwe katika mpango maalum wa kibiashara za utabiri “official oracle business" lakini hata hivyo aligoma
Kabla ya kifo chake ameacha utabiri mwingine wa nani atakayefanikiwa kupata nafasi ya kuandaa fainali zijazo za mwaka 2018 ambapo Marehemu Pweza Paul ameitabiria Uingereza kufanikiwa kupata nafasi hiyo huku majibu yake yakitarajiwa kutolewa Mwezi Desemba pale kamati ya Fifa itakapo keti huko Zurich Uswiz.



No comments:

Post a Comment