KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, October 26, 2010

Hispania yajaza wachezaji katika kuelekea kutajwa washindi wa tuzo ya fifa Jumla ya wachezaji saba wa kikosi cha ushindi cha kombe la dunia cha Hispania, wametajwa katika orodha fupi ya wachezaji wanao wania tuzo ya Fifa ya Ballon d'Or award.
Andres Iniesta ambaye alifunga bao la ushindi katika mchezo wa fainali dhidi ya Uholanzi ametajwa katika orodha hiyo sambamba na wenzake wa timu moja ya Barcelona Xavi, Carles Puyol and David Villa.
Wengine ni kutoka klabu ya Real Madrid ametajwa mlinda mlango Iker Casillas na Xabi Alonso.
Cesc Fabregas wa Arsena na timu ya taifa ya Hispania ametajwa kuwania tuzo hiyo huku mwingine akiwa ni mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Ivory Coast Didier Drogba na Asamoah Gyan wa Sunderland na timu ya taifa ya Ghana lakini jambo la kushangaza ni kukosekana kwa mchezaji hata mmoja toka Uingereza licha ya ligi zao kuonekana kuwa na mvuto mno duniani
Kumbuka tuzo hiyo iliasisiwa barani Ulaya lakini kadri muda ulivyozidi kusonga mbele na kuonekana kuwa na maana zaidi ndipo ilipochukuliwa na shirikisho la kandanda duniani Fifa na heshima kuwa ni ya dunia nzima.
Wesley Sneijder anapewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo akiwa tayari amesha shinda mataji matatu
Wachezaji wa zamani wa Inter Milan ambayo walikuwepo katika kikosi cha ushindi wa mataji ya Italian League ,Italian Cup na ligi ya mabingwa wamo ndani ya orodha hiyo na hawa ni Samuel Eto'o, Julio Cesar, Maicon na Wesley Sneijder.
Kocha msemaji na mwenye majitapo ya mara kwa mara ambaye kwasasa amekuwa kidogo mkimya Jose Mourinho ambaye alikuwa akiongoza timu yenye mafanikio ya Italia ya Inter Milan sasa anaungana na wengine kama Carlo Ancelotti wa Chelsea, meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson na Arsene Wenger wa Arsenal katika orodha fupi ya kuwania tuzo ya kocha wa mwaka.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza Kelly Smith na kocha Hope Powell wametajwa kuwania tuzo ya mwaka kwa upande wa tuzo za wanawake.
Washindi wa tuzo hizo watatangzwa baada ya maamuzi ya kura kufanywa na manahodha na makocha wa timu za taifa pamoja na wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya habari watakao teuliwa na jarida la France Football magazine.
Washindi watatangazwa januari 10 huko Zurich Uzwiz yaliko makao makuu ya FIFA.
Wachezaji
Xabi Alonso (Spain), Daniel Alves (Brazil), Iker Casillas (Spain), Cristiano Ronaldo (Portugal), Didier Drogba (Ivory Coast), Samuel Eto'o (Cameroon), Cesc Fabregas (Spain), Diego Forlan (Uruguay), Asamoah Gyan (Ghana), Andres Iniesta (Spain), Julio Cesar (Brazil), Miroslav Klose (Germany), Philipp Lahm (Germany), Maicon (Brazil), Lionel Messi (Argentina), Thomas Muller (Germany), Mesut Ozil (Germany), Carles Puyol (Spain), Arjen Robben (Holland), Bastian Schweinsteiger (Germany), Wesley Sneijder (Holland), David Villa (Spain) and Xavi (Spain).

Makocha
Carlo Ancelotti (Chelsea), Vicente del Bosque (Spain), Sir Alex Ferguson (Manchester United), Pep Guardiola (FC Barcelona), Joachim Loew (Germany), Jose Mourinho (Inter Milan/Real Madrid), Oscar Tabarez (Uruguay), Louis Van Gaal (Bayern Munich), Bert van Marwijk (Holland) and Arsene Wenger (Arsenal).
Previous Ballon d'Or winners:
1956 - Stanley Matthews (England), 1957 - Alfredo di Stefano (Spain), 1958 - Raymond Kopa (France), 1959 - Alfredo di Stefano (Spain), 1960 - Luis Suarez (Spain), 1961 - Omar Sivori (Italy), 1962 - Josef Masopust (Czechoslovakia), 1963 - Lev Yashin (USSR), 1964 - Denis Law (Scotland), 1965 - Eusebio (Portugal), 1966 - Bobby Charlton (England), 1967 - Florian Albert (Hungary), 1968 - George Best (Northern Ireland), 1969 - Gianni Rivera (Italy), 1970 - Gerd Mueller (West Germany), 1971 - Johan Cruyff (Netherlands), 1972 - Franz Beckenbauer (West Germany), 1973 - Johan Cruyff (Netherlands), 1974 - Johan Cruyff (Netherlands), 1975 - Oleg Blokhin (USSR), 1976 - Franz Beckenbauer (West Germany), 1977 - Allan Simonsen (Denmark), 1978 - Kevin Keegan (England), 1979 - Kevin Keegan (England), 1980 - Karl-Heinz Rummenigge (West Germany), 1981 - Karl-Heinz Rummenigge (West Germany), 1982 - Paolo Rossi (Italy), 1983 - Michel Platini (France), 1984 - Platini, 1985 - Platini, 1986 - Igor Belanov (USSR), 1987 - Ruud Gullit (Netherlands), 1988 - Marco van Basten (Netherlands), 1989 - Marco van Basten (Netherlands), 1990 - Lothar Matthaus (Germany), 1991 - Jean-Pierre Papin (France), 1992 - Van Basten, 1993 - Roberto Baggio (Italy), 1994 - Hristo Stoichkov (Bulgaria), 1995 - George Weah (Liberia), 1996 - Matthias, Sammer (Germany), 1997 - Ronaldo (Brazil), 1998 - Zinedine Zidane (France), 1999 - Rivaldo (Brazil), 2000 - Luis Figo (Portugal), 2001 - Michael Owen (England), 2002 - Ronaldo, 2003 - Pavel Nedved (Czech Republic), 2004 - Andriy Shevchenko (Ukraine), 2005 - Ronaldinho (Brazil), 2006 - Fabio Cannavaro (Italy), 2007 - Kaka (Brazil), 2008 - Cristiano Ronaldo (Portugal), 2009 - Lionel Messi (Argentina

No comments:

Post a Comment