Wachezaji
ngwinji wa mabingwa watetezi wa ulaya Hispania Busquets na Xavi wamesema wanayo
dawa ya kumzima mshambuliaji wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo katika
mchezo wa nusu fainali wa michuano ya Ulaya utakao pigwa jumatano.
Roja watakutana
na Seleccao wakati ambapo Sergio Busquets na Xavi wakiamini kuwa wanajua mbinu
ya kupunguza makali ya Cristiano Ronaldo katika mchezo huo.
Ronaldo alifunga
goli zuri la kichwa lililoifungisha virago jamhuri ya Czech Republic kwenye
robo fainali na kuwasogeza Seleccao kwenye nusu fainali.
Wakati
wakali hao wa Barcelona wakiwa na hadhari kubwa kwa Ronaldo pia wanamatumaini
wana uwezo wao binafsi wa kumpoteza mshambuliaji huyo wa Real Madrid man.
"si
kama ni mchezo baina ya Barcelona na Madrid ni Hispania dhidi ya Ureno na sote
tunajua ukubwa wa uchezaji wa Cristiano.
"atakuwa
mara zote anapumuliwa na na Alvaro Arbeloa na Alvaro anamjua vizuri kuliko mtu
yoyote wote wanachezea Real Madrid. Lakini kumnyima nafasi ya kucheza mchezaji
kama huyu inahitajika timu nzima kushirikiana."
Xavi anaamini
yeye na wenzake wa sehemu ya ulinzi wataziba nafasi ya kucheza mchezaji huyu wa
zamani bora wa dunia kufanya vitu vyake.
"tunapaswa
kuwa tayari."anasema Xavi.
"tutajaribu kuzuia pia kumnyima raha Cristiano
na kumnyima nafasi hata ya kugeuka."
Cesc
Fabregas ana ulinganisha mchezo wa Hispania dhidi ya Ureno wa nusu fainali ya Euro
2012 kuwa kama Clasico kati ya Barcelona na Real Madrid.
Hispania imeelekea
katika nusu fainali katika hali ya kujaribu kutete taji lao lakini huenda
ikakutana na jaribio zito la kufanya hivyo dhidi ya shughuli pevu ya Ureno
itakayo ongozwa na Cristiano Ronaldo.
Fabregas ameielezea
Ureno kama hatari zaidi katika eneo la ushambuliaji na wachezaji karibu wengi
toka kila upande wakitoka katika vilabu viwili pinzani nchini Hispania Barca na
Real itakuwa kama ni El Clasico.
Fabrigas
anasema
"Ureno
ni moja kati ya timu ngumu, wanalinda vizuri na hatari katika kushambulia, ni
kama ilivyo Real Madrid na tupaswa kuwa katika kiwango katika mchezo huo.
“unaweza fananisha Real Madrid dhidi ya Barcelona
katika mazingira ya aina ya uchezaji wa timu.
No comments:
Post a Comment