Hii ndio kamati ya uchaguzi ya TFF |
Kuelekea uchaguzi wa klabu Yanga ambao umepangwa kufanyika Julay 15, wagombea wawili wa nafasi za uongozi ndani yha klabu hiyo wamepingwa kugombea Uongozi huku mfanyabiashara maarufu Yusufu Manji akiwekewa sababu 14 za kupingwa kuwania nafasi ya Mwenyekiti ya klabu hiyo.
Taarifa zilizo ifikia Rockersports kupitia msemaji wa TFF Bornface Wambura zimesema Manji amepingwa na mmoja wa wanachama wa klabu hiyo ambaye hata hivyo akishindwa kutaja jina lake.
Mgombea mwingine aliyepigwa ni Yono Kevela na hoja ikiwa ni sababu gani ilipelekea Kamati ya uchaguzi ya Yanga kumpitisha.
kwa mujibu wa Wambura ni kwamba kinachosubiriwa ni kamati ya uchaguzi ya TFF kuketi kama kamati ya rufaa kupitia mapingamizi hayo chini ya mwenyekiti wake Deo Lyato ambaye kwasasa inaarifiwa kuwa yuko nje ya nchi lakini kikao hicho kikitarajiwa kufanyika tarehe 29 june 2012.
Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya Yanga Jaji mkwawa. |
Mgombea wa nafasi ya mwenyekiti Yanga Yusufu Manji. |
No comments:
Post a Comment