KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, November 3, 2012

VAN PERSIE AWAVUNJIA HESHIMA ARSENAL HII LEO NA CESAR AWATAKA INTER KUONDOA HOFU DHIDI YA KIBIBI KIZEE CHA TURIN.



Julio Cesar: Inter ndiyo mpinzani pekee wa Juventus kuwania Scudettol.
Julio Cesar anaamini kuwa Inter Milan ndiyo mpinzani pekee wa Juventus katika mbio za kusaka taji la ligi kuu ya nchini Italia ‘Scudetto’ msimu huu wakati wakielekea katika mchezo mkubwa maarufu kama ‘Derby d'Italia’ usiku huu.

Nerazzurri kwasasa wako katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya nchini Italia Serie A, ikiwa na alama nne nyuma ya mabingwa watetezsi hao.

Mlinda mlango huyo mzaliwa wa Brazil kwasasa akiwa QPR, amesisitiza kuwa klabu yake ya zamani inapaswa kuingia katika mchezo huyo huku wakiondoa hofu dhidi ya bibi kizee cha Turin.
Amenukuliwa na Gazzetta dello Sport akisema,
"Juve lazima ishambuliwe katika mchezo huo,kwanini wasishambuliwe? Inter anaonekana ndio mpinzani mkubwa pengine mpinzani pekee. Inawezekana hata zaidi ya Napoli, ambao hawako vizuri kama Inter.

"nilikuwa nma muda wa kujifunza filosofia ya Andrea  Stramaccioni, nilitaka kufanya naye kazi zaidi. Ana njia nzuri ya kuona mchezo na kwa unyenyekevu ana msikia kila mtu lakini hana woga.

Cesar aliondoka Giuseppe Meazza majira ya kiangazi na nafasi yake ilichukuliwa na Samir Handanovic, ambaye alitokea Udinese.
Robin van Persie awamaliza Arsenal.
 
 Mshambuliaji wa zamani wa washika mitutu wa England Robin van Persie hii leo alikuwa ni mwiba mchungu kwa klabu yake hiyo ya zamani ya Arsenal, kufuatia hii leo kuwafunga jamaa zake katika mchezo ulimalizika kwa Mashetani wekundu Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 mchezo ulipigwa katika dimba la Old Trafford.

Ilimchukua mduchi huyo dakika tatu kuandika bao la uongozi ukiwa ni mchezo wake wa kwanza kucheza dhidi ya timu yake ya zamani ambayo aliihama kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 24 majira ya kiangazi, kabla ya Wayne Rooney kukosa penati ambayo pengine ingeandika bao la pili kwa United.

Patrice Evra aliiandikia United bao la pili kunako dakika ya 66 ya mchezo bao ambalo ndilo lilikuwa bao la ushindi ambalo limeipeleka moja kwa moja United katika uongozi wa ligi ya soka nchini England maarufu kama ‘Premier League’ ndani ya muda mfupi wakati yakisubiriwa matokeo ya mchezo kati ya Chelsea dhidi ya  Swansea.

Arsenal ililazimika kucheza ikiwa pungufu ya mchezaji mmoja katika dakika 21 za mwisho wa mchezo kufuatia  Jack Wilshere kutolewa nje ya uwanja baada ya kupewa kadi ya pili ya manjano kabla ya Santi Cazorla kufunga goli la kufutia machozi ukiwa ni mpira wa mwisho katika mchezo huo.

Mashabiki takribani 3,000 waliokuwa ndani ya Old Trafford jioni ya leo walikuwa wakionyesha hasira zao waziwazi huku wakiimba nyimbo ambazo zilimlenga mtendaji mkuu wa Gunners Ivan Gazidis kwa maneno ya ‘tunaitaka Arsenal yetu irejee’.

No comments:

Post a Comment