KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, November 3, 2012

Hatimaye Thiago wa Messi amezaliwa

Thiago Messi
Jezi maalum ya Thiago
Mshambuliaji wa Barcelona  Lionel Messi hatimaye amekuwa baba kwa mara ya kwanza baada ya mpenzi wake Antonella Roccuzzo kufanikiwa kujifungua salama mtoto wa kiume ambaye alikuwa amekwisha kupewa jina la Thiago.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 jana alipewa ruhusa ya kutokuhudhuria mazoezi na kwenda kuungana na mpenzi kuelekea katika hospitali ya USP Dexeus tayari kumpokea Thiago.
Baada ya masaa kadhaa mtoto huyo wa kiume alizaliwa majira ya saa 11 joini huku Roccuzzo akizungukwa na ndugu na marafiki wakiwemo wazazi wa Messi, Jorge na Celia.

Licha ya kufanikiwa kupata mtoto huyo bado Messi amejumuishwa katika kikosi cha Barca kitakacho kuwa dimbani usiku wa leo dhidi ya Celta Vigo.

No comments:

Post a Comment