KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, November 3, 2012

AL HILAL YA SUDAN YAJIWEKA VIZURI MCHEZO WA KWANZA KOMBE LA SHIRIKISHO



Al Hilal ya sudan imejiweka katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya jana kufanikiwa kuichapa Djoliba ya Mali kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo.

Mabao ya Hilal yaliwekwa kimiani na Ibrahima Sane na  Mudathir Careca.

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Hilal ilishindwa mara tatu kupenya katika hatua hiyo katika michuano ya vilabu bingwa Afrika na mara moja katiki mochuano ya kombe la shirikisho.
Walimaliza katika nafasi ya pili katika kundi A na hivyo kujikuta wakikutana na Djoliba, ambao waliibuka washindi wa kundi B.

AC Leopards watakuwa wenyeji wa Al Merreikh katika mchezo wa nusu fainali nyingine itakayopigwa hapo kesho.

No comments:

Post a Comment