![]() |
Tajiri wa Forbes Floyd Mayweather |
Floyd Mayweather amefanikiwa kumshinda Tiger
Woods kutengeneza pesa katika kipindi cha mwaka jana kwa mujibu wa orodha ya
inayo andaliwa na jarida la Forbes.
Forbes limekuwa kila mwaka likiandaa
orodha ndefu ya wanamichezo wanaolipwa pesa nyingi duniani ambapo kwa mwaka
jana jarida hilo limeonyesha kuwa Mayweather amekuwa ni mwenye thamani zaidi na
kumshinda mchezaji golf mashuhuri duniani Tiger.
Bondia Mayweather kwasasa anatumikia
adhabu ya kifungo cha miaka 3 kwa kutumia lugha ya matusi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizo toka hii leo
zimearifu kuwa Mayweather ametengeneza kipato cha dolari za kimarekani $85m
(£54.25m) kutokana na mafanikio ya kutengeneza promotion ya michezo yake.
Mwasisi katika mchezo wa Golf Tiger Woods ameshuka
na kukusanya dolari za kimarekani $59.4m (£37.92m) ilhali bondoa mwingine Manny
Pacquiao akipanda kimapato na kufikisha jumla ya dolari $62m (£39.57m).
![]() |
Tiger Woods |
Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza
David Beckham kwa mujibu wa orodha hiyo yupo katika nafasi ya nane.
Hata hivyo yeye ndiye mwanasoka anaye
tengeneza pesa nyingi zaidi kiasi cha dolari $46m (£29.36m).
Orodha kamili mpaka nafasi ya kumi
1 Floyd Mayweather $85m (£54.25m)
2 Manny Pacquiao $62m (£39.57m)
3 Tiger Woods $59.4m (£37.92m)
4 LeBron James $53m (£33.84m)
5 Roger Federer $52.7m (£33.64)
6 Kobe Bryant $52.3m (£33.38m)
7 Phil Mickelson $47.8m (£30.51m)
8 David Beckham $46m (£29.36m)
9 Cristiano Ronaldo $42.5m (£27.10m)
10 Peyton Manning $42.4m (£27.06m)
Woods amekuwa akiongoza katika orodha ya Forbes
tangu mwaka 2001 lakini akashuka kimapato kwa dolari $16m (£10.21m) kuanzia
mwaka jana na kushuka kwa kiwango cha nusu ya kipato chake cha mwaka 2009. Taarifa
zinasema huenda kashfa ya ngono imechangia.
Nyota wa kikapu wa Miami Heat LeBron James
yuko katika nafasi ya nne amekusanya $53m (£33.84m),ikiwa ni zaidi kwa wacheza
13 katika orodha hiyo na mcheza Tennis raia wa Uswiss Roger Federer akiwa
katika nafasi ya tano baada ya kuweza kulipwa dolari $52.7m (£33.64m).
Mcheza soka mwingine mchezaji wa Real
Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amepanda baada ya
kutengeneza dolari $42.5m (£27.10m) .
Fernando Alonso ameingia baada ya
mafanikio ya michezo ya mashindano ya magari ya Formula 1 ameshika nafasi ya 19
kwa kuingiza dolari $29.4m (£18.7m).
Mwendesha magari toka MotoGP Valentino
Rossi yuko katika nafasi ya 20 na mshindi mara saba wa mashindano ya magari ya Formular
1 Michael Schumacher yeye yuko katika nafasi ya 21wakati ambapo Lewis Hamilton akiwa
katika nafasi 24 baada ya kukusanya dolari $17.8m (£11.3m) huku dolari $15.9m
(£10.1m) zikitokana na mshahara wa McLaren.
Mshambuliaji wa Manchester United na timu
ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney yuko katika nafasi ya 37 kutokana na kipato
cha dolari $15.5m (£9.8m) ilhali Luke Donald mchezaji golf namba moja kwasasa
akiwa katika nafasi ya 48 kufuatia kukusanya dolari $14.17m (£9m).
Wanawake wawili pekee walio katika orodha
ni mcheza tenis raia wa Russian Maria Sharapova yuko katika nafasi ya 26
kutokana na kipato cha dolari $27.9m (£17.79m) na mwingine ni Li Na raia wa China ambaye ni bingwa wa mwaka jana wa
michuano ya wazi ya tenis ya French champion yeye yuko katika nafasi ya 81
kutokana na kipato chake kufikia dolari $18.4m (£11.72m) hususani baada ya kuwa
mzaliwa wa bara la Asia pekee kushinda taji la mchezo wa tenis la Grand Slam kwa
mchezaji mmoja mmoja.
No comments:
Post a Comment