Rais wa
shirikisho la soka nchini Ivory Coast ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji
ya shirikisho la soka duniani FIFA Jacques Anouma ameshindwa rufaa yake ya
akipinga sheria iliyomzuia kushirikia uchaguzi wa Rais wa shirikisho la soka
barani Afrika CAF akiwania nafasi ya urais wa shirikisho hilo katika uchaguzi
ambao umepangwa kufanyika wiki ijayo.
Mahakama ya
kimataifa ya michezo (CAS) hapo jana imesema kuwa imekubaliana na mabadilioko
yaliyofanywa na CAF mwezi septemba mwaka jana ambayo yanataka wagombea wa
nafasi ya Urais watoke katika kamati ya utendaji ya shirikisho hilo.
Taarifa
iliyotolewa na CAS hapo jana imesema kuwa mabadiliko yaliyofanywa na CAF mwezi
septemba mwaka jana ni halali kutumika katika uchaguzi uchaguzi huo na kwamba
kwa mujibu wa mabadiliko hayo ni kwamba Anouma amekosa sifa hiyo muhimu ya
ujumbe wa kamati ya utendaji wa shirikisho hilo la soka barani Afrika.
Rais wa sasa
wa CAF Issa Hayatou atakuwa akiingia katika uchaguzi bila mpinzani akiwania
nafasi ya Rais kwa kipindi kingine cha miaka minne ya uongozi wa shirikisho
hilo la soka barani Afrika ambao utafanyika jijini Marrakech nchini Morocco
jumapili.
No comments:
Post a Comment